Sauti za Vijana
Kifo Siyo Mwisho
Kielelezo na Katelyn Budge
Mama yangu alilazwa hospitalini akiwa na kiharusi. Ilitushtua, na nilijiuliza kwa nini Mungu aliruhusu hili litokee.
Licha ya wasiwasi wetu, hatukupoteza imani. Tulijua kwamba angepona. Alikuwa SAWA hadi miezi michache baadaye wakati alipopatwa na kiharusi kingine. Hakuweza kutembea au kuzungumza na alipata wakati mgumu kula. Tuliendelea kusali kwa ajili ya msaada kutoka kwa Mungu.
Mama yangu alipigana na hali hii hadi alipofariki. Ninajua si kwamba Mungu hakuweza kumponya, lakini ilikuwa ni mapenzi Yake kwamba arudi Kwake. Ninajua kwamba kama ninaishi maisha yangu kulingana na amri za Bwana, ninaweza kuungana tena na yeye na familia yangu. Ninajua kwamba kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi wetu, tutafufuliwa. Kifo siyo mwisho kwetu.
Anicet P., umri miaka 17, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Hufurahia kusikiliza muziki, kutumia muda pamoja na familia, na kusoma maandiko na vitabu vizuri.