Unganika
Danic L.
17, Negeri Sembilan, Malaysia
Picha na Clayton Chan
Siku nyingi, ninahisi kama mimi si mzuri vya kutosha na kama ninaweza kuwa wa kukatisha tamaa. Lakini daima ninafikiria juu ya kile Mungu anachofikiria juu yangu. Nakumbuka asili yangu ya kiungu, uwezekano wangu wa kiungu, na hiyo ni nguvu na nanga kwangu.
Ninacheza mpira wa vinyoya, na baada ya kucheza mashindano na kupoteza, hasa kwa mtu unayedhania kuwa unaweza kumfunga, unajisikia kushindwa sana. Nyakati hizo ninamfikiria Mungu akiwa pale kwa ajili yangu, na inanipa nguvu ya kuendelea kusonga mbele.
Unaweza kuhisi upendo wa Mungu unapomtegemea Yeye. Yeye daima yupo hapo kwa ajili yako, na unaweza kuwa na nguvu ya kiungu ambayo Yeye anaweza kukupatia.
Yesu Kristo Ni Mwokozi Wetu. Alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. Upendo ambao Yeye alihitaji kwa hiari kufa kwa ajili yetu—nadhani ni upendo ambao ni vigumu kuuelezea. Ni ya thamani sana na yenye nguvu.