2025
Faraja ya Mkutano
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Septemba 2025


Sauti za Vijana

Faraja ya Mkutano Mkuu

msichana akizungumza kwenye mimbari

Kielelezo na Katelyn Budge

Niliombwa kuzungumza katika mkutano wa kigingi. Lakini nilidhani nisingekuwa na muda wa kujiandaa kwa vile majukumu ya shule yalikuwa mbeleni.

Wakati nikiwa bado sijaamua kama ningezungumza, kukawa na mkutano mkuu. Kuonesha imani katika Mwokozi wetu, Yesu Kristo, kunatusaidia kushinda kukatishwa tamaa bila kujali ni vikwazo gani tunakabiliana navyo.”

Nilikumbuka jinsi Bwana alivyonisaidia kutimiza majukumu yangu hapo awali. Nilipounganisha uzoefu wangu binafsi na ushuhuda wa Mzee Cook, nilielewa kwamba ningewezeshwa kukamilisha hotuba yangu ya mkutano wa kigingi bila woga.

Ninashuhudia kwamba ninapohisi wasiwasi au woga, Kristo atanivuvia kupitia maneno ya manabii na viongozi wengine wa Kanisa, maandiko, na watu wanaonizunguka.

msichana

Eru M., umri miaka 17, Mkoa wa Gunma, Japani

Anapenda kupiga ala za muziki na kuangalia picha za zamani na video ili kukumbuka kuhusu kumbukumbu.