Ishara za Ujio wa Pili: Hakuna Sababu ya Hofu
Baadhi ya mambo makubwa yametabiriwa kabla ya Mwokozi kuja tena. Lakini una sababu nzuri za kutoogopa.
Anakuja Tena Kutawala na Kuongoza, na Mary RL Sauer
Mwokozi Wetu, Yesu Kristo, atakuja tena. Alifundisha ukweli huu kwa uwazi kabisa (ona Mathayo 24). Watu wengi wangependa kujua lini hili litatokea, lakini Yesu alisema, “katika siku ile na saa hajui mtu yeyote, hapana, si malaika wa mbinguni, bali Baba yangu pekee” (Mathayo 24:36).
Hata hivyo, Bwana amefunua ishara kadhaa ambazo zitatangulia Ujio Wake wa Pili. Mengi ya haya ni ya kusisimua na ya kupendeza, kama vile Urejesho wa injili, kuja kwa Kitabu cha Mormoni, na kukusanyika kwa Israeli.
Lakini kisha kuna … ishara zingine. Kwa mfano:
-
Ishara mbinguni (ikijumuisha jua, mwezi, na nyota) na duniani (ikijumuisha moto, dhoruba, na mivuke ya moshi).
Hayo yote yanaweza kusikika kama yenye kutisha. Kwa kweli, Mwokozi alisema kwamba katika siku za mwisho, mioyo ya watu wengi itazimia kwa sababu ya hofu.
Sasa, pengine unatazama matatizo ulimwenguni kote, pamoja na majaribu binafsi unayokabiliana nayo, na kuhisi kuzidiwa na wasiwasi. Pengine unajiuliza unatakiwa kutazamia nini kama mambo yatakuwa ya kuogopesha na magumu zaidi kuongoza kwenye Ujio wa Pili.
Lakini hivi sivyo ambavyo Yesu Kristo angetaka wewe—mmoja wa wanafunzi Wake—utarajie kurudi Kwake.
Ujumbe wa Bwana kwa Wanafunzi Wake
Hata pamoja na misukosuko yote ya siku za mwisho, Mwokozi amewaambia wanafunzi Wake, “Msifadhaike.” Kwa nini? Kwa sababu “kwani haya yote yatakapokuja kutukia, ninyi muweze kujua kwamba ahadi ambazo zimefanywa kwenu zitatimizwa”(Mafundisho na Maagano 45:35).
Yesu Kristo ametuambia “tusiogope” (Mafundisho na Maagano 50:41) na “jipeni moyo” (Mafundisho na Maagano 61:36). Kwa hiyo, badala ya kufokasi kwenye majanga yajayo, inaweza kuwa bora kubadili fokasi yetu.
Hapa kuna njia tatu muhimu ambazo unaweza kuzitumia ili “usiogope,” kutazamia Ujio wa Pili mtukufu, na kusema, pamoja na Yohana Mfunuzi, “Na uje, Bwana Yesu” (Ufunuo 22:20).
1. Mtegemee Nabii
Mwokozi alionya kwamba kutakuwa na Kristo wengi wa uongo na manabii wengi wa uongo kabla ya kuja Kwake ambao wangewadanganya watu wengi. Kote karibu nasi, kuna sauti kubwa, zenye kukanganya, na hasi zinazojaribu kutupotosha. Katika siku za mwisho, Shetani “atatawala katika mioyo ya watoto wa watu, na kuwachochea kuwa na hasira dhidi ya yaliyo mema” (2 Nefi 28:20). Hata wateule watasogezwa mbali na ukweli.
Lakini Bwana ametupa msaada mkubwa. Amewaita manabii kutubariki na kutuongoza. Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili hawatatupotosha na hawawezi kutupotosha. Mwokozi alisema “Iwe kwa sauti yangu mwenyewe au kwa sauti ya watumishi wangu, yote ni sawa” (Mafundisho na Maagano 1:38). Unaweza kumwomba Baba wa Mbinguni Roho Mtakatifu ili kuthibitisha kweli wanazofundisha, kama vile mafundisho ya hivi karibuni ya Rais Russell M. Nelson: “Mambo mazuri zaidi bado yako mbeleni, … kwa sababu Mwokozi anakuja tena!” Na: “Anajitayarisha kuja tena. Na sisi vile vile tujiandae kumpokea Yeye.”
Na unapofuata mafundisho yao “katika uvumilivu wote na imani” (Mafundisho na Maagano 21:5), unaweza kuona jinsi yanavyobariki maisha yako.
Mzee Allen D. Haynie wa wale Sabini amesema: “Nilipokuwa mtoto, unabii wa siku za mwisho ulinitisha na kunisababishia kuomba kwamba Ujio wa Pili usingekuja katika maisha yangu. … Lakini sasa ninasali kinyume chake. …
“…Hatuhitaji kuwa na hofu. Mafundisho na kanuni tunazopaswa kufuata ili tunusurike kiroho na kustahimili kimwili vinapatikana katika maneno ya nabii aliye hai.”
Unapofuata mwongozo wa manabii na mitume, hofu yako itatoa njia kwa imani, tumaini, na shangwe.
Simama katika Mahali Patakatifu
Mwokozi amesema kwamba katikati ya majanga ya siku za mwisho, “wanafunzi wangu watasimama katika mahali patakatifu, na hawataondoshwa” (Mafundisho na Maagano 45:32). Sehemu hizi takatifu ni pamoja na nyumba zetu, nyumba za mikutano, na mahekalu.
Kuhusu mahekalu, Rais Nelson amefundisha kwamba “bima yetu iliyo salama zaidi ni kuendelea kuwa wastahili wa kuingia katika nyumba Yake takatifu.” Na “ongezeko la muda hekaluni litatusaidia kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili.”
Jioni, na Yongsung Kim
3. Kuuandaa Ulimwengu
Jukumu moja Kanisa la Yesu Kristo linafanya katika siku za mwisho ni kusaidia kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya ujio Wake. Na unaweza kusaidia kwa kushiriki katika kazi Yake.
Unaweza kushiriki injili na wengine na kusaidia kuleta nuru na ukweli wa Mungu kwa wale “ambao wamezuiliwa kuupata ukweli kwa sababu hawajui wapi pa kuupata” (Mafundisho na Maagano 123:12).
Unaweza pia kufanya ubatizo hekaluni kwa niaba ya wale walio upande mwingine wa pazia ambao waliishi na “walikufa bila ufahamu wa injili [hii], ambao wangeipokea” (Mafundisho na Maagano 137:7).
Kukiwa na mambo mengi hasi ulimwenguni, unaweza kuwa nuru kwa wengine na kusaidia kuleta uponyaji ulimwenguni. Unaweza kusaidia kuwaandaa watu ambao Mwokozi anaweza kuja kwao ambao watakuwa tayari kumpokea Yeye.
Hilo ni jukumu kubwa na kitu cha kupendeza kutazamia.