Kwenye Hoja
Je, ni udanganyifu kunakili kutoka kwenye intaneti au akili mnemba kwa ajili ya kazi za shule?
Jibu fupi ni ndiyo.
Teknolojia huweka taarifa kiuhalisia kwenye ncha za vidole vyako. Ni zana kubwa kwa ajili ya utafiti na kujifunza. Lakini swala la kunakili kutoka kwenye intaneti au akili mnemba kwa ajili ya kazi za shule ni chini ya kile kinachofaa. Ni zaidi kuhusu madhumuni ya elimu yako ni nini hasa.
Baba wa Mbinguni anataka binti zake na wanawe siku zote wawe wanajifunza. … Elimu … ni sehemu ya lengo lako la milele la kuwa zaidi kama Baba wa Mbinguni” (Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi [2022], 31). Aina hii ya elimu ni kuhusu kukuza akili yako na maarifa yako. Sio kuhusu kile unachoweza kukwepa ili kutimiza mahitaji ya chini.
Na juu ya swali la kudanganya: Kama shule yako au mwalimu anakuambia usinakili kutoka intaneti au akili mnemba, basi usifanye hivyo. Kama mwalimu wako anakupangia wewe kuandika kitu fulani, basi wewe kiandike. Kama huna uhakika nini kinaruhusiwa katika kazi yoyote uliyopangiwa, muulize mwalimu wako.
“Kuishi kwa uadilifu inamaanisha kwamba unapenda ukweli kwa moyo wako wote—zaidi kuliko unavyopenda … urahisi” (Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi, 31).