2025
Baada ya Maisha Haya: Majibu kwa Baadhi ya Maswali
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ya Julai 2025


Baada ya Maisha Haya

Majibu kwa Baadhi ya Maswali

Mpango wa Baba wa Mbinguni unaweza kutupatia mtazamo na amani kuhusu maisha baada ya kifo.

ngazi katika mawingu

Kielelezo na Thomas Arnaud

Je, ni nini kitatokea baada ya kufa kwetu?

Hili labda ni swali katika dini zote. Majibu tuliyonayo kupitia Yesu Kristo na injili Yake ni yenye nguvu. Maisha haya sio mwisho Kwa sababu Yesu Kristo alifufuliwa, roho zetu zitaungana tena na miili yetu, na sisi sote tutafufuka siku moja.

Bila shaka, kuna maelezo mengine kuhusu maisha baada ya kifo ambayo yamekuja kwetu kupitia ufunuo wa siku hizi ambao unaweza kujibu maswali mengine tunayoweza kuwa nayo. Hapa kuna baadhi ya maswali kama hayo, pamoja na baadhi ya majibu mafupi.

Miili ya kiroho ikoje?

Roho ni aina ya maada, ila tu ni “nzuri zaidi au safi sana” (Mafundisho na Maagano 131:7). Miili ya kiroho inaonekana kama miili ya binadamu mtu mzima.

Ulimwengu wa kiroho uko wapi?

Hapa, kote kutuzunguka sisi.

Nini kinaendelea katika ulimwengu wa roho?

Miongoni mwa mambo mengine, roho ambazo zimekubali injili zimepangwa kuhubiri injili kwa roho ambao hawajaikubali injili. Roho hizo zinaweza kuchagua kuikubali au kuikataa.

Miili iliyofufuka inafananaje?

Miili iliyofufuka haiwezi kufa, ni miili ya nyama na mifupa, na ni mikamilifu. Ni mitukufu na mizuri. “Hakuna kitu kizuri zaidi cha kutazama kuliko mwanaume au mwanamke aliyefufuka.”

Nini kinaendelea katika ufalme wa selestia?

Wale walio katika daraja la juu kabisa la ufalme wa selestia wanakuwa kama Baba yetu wa Mbinguni na kupata utimilifu wa shangwe. Wote wanapokea vyote ambavyo Baba anavyo. Wanashiriki katika kazi na utukufu Wake. Waliunganishwa katika ndoa ya milele na sasa wanaishi katika familia za milele, wakiwa na watoto wao wa kiroho.

Vipi kuhusu watu ambao kamwe hawaoi au kuolewa katika maisha haya?

Baba wa Mbinguni kwa ukamilifu ni mwenye haki na huruma. Bwana ameahidi kwamba katika maisha ya milele hakuna baraka watakayonyimwa wana na mabinti Zake wanaotii amri, ni wa kweli katika maagano yao, na kutamani kile kilicho cha haki.”

Wazazi wangu waliunganishwa hekaluni, lakini sasa wametalikiana. Nimeunganishwa na nani?

Yawezekana kuwa “umezaliwa katika agano” (ambalo ni, kuzaliwa baada ya wazazi wako kuunganishwa hekaluni), au yawezekana kuwa umeunganishwa kwa wazazi wako hekaluni baada ya wao kuwa wameunganishwa. Kwa hali yoyote, baraka zako zinabaki kuwa hai hata kama wazazi wako watachagua kutalikiana na kufutwa kwa kuunganishwa kwao.

Chaguzi za wazazi wako haziathiri baraka zako. Kitu muhimu ni kwako wewe kubaki mwaminifu na kutafuta baraka za hekaluni wewe mwenyewe. Kuhusu uhusiano wa familia yako, unapaswa “kumwamini Bwana na kutafuta faraja Yake,” ukijua kwamba “Baba wa Mbinguni atahakikisha kwamba kila mtu anapokea kila baraka ambayo matamanio yake na machaguo yake huruhusu.”

Ni nini hutokea kwa watu wanaokufa kwa kujiua?

Hatujui nini kinatokea kwa watu wanaokufa kwa kujiua, na hatuwezi kuwahukumu (kama vile ilivyo kwa watu wote, hatimaye). “Licha ya juhudi nzuri za wapendwa wetu, viongozi na wataalamu, kujiua si mara zote kunazuilika. …

“Siyo sahihi kwa mtu kujitoa uhai wake. Hata hivyo, Mungu peke Yake anaweza kuhukumu mawazo ya mtu, vitendo na kiwango cha uwajibikaji (ona 1 Samweli 16:7; Mafundisho na Maagano 137:9). …

Wale ambao wamempoteza mpendwa wao kwa kujiua wanaweza kupata tumaini na uponyaji katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake.”.

Mihutasari

  1. Ona Etheri 3:16; Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (1998), 131–32.

  2. Ona Teachings of Presidents of the Church: Brigham Young (1997), 279.

  3. (Ona Mafundisho na Maagano 138.)

  4. Ona Alma 11:45.

  5. Ona Luka 24:39.

  6. Ona Alma 11:43.

  7. Lorenzo Snow, The Teachings of Lorenzo Snow, ed. Clyde J. Williams [1996], 99.

  8. Ona Musa 1:39.

  9. Ona Zaburi 16:11; 3 Nefi 28:10; Mafundisho na Maagano 76:59, 62; 130:2; 132:19–23.

  10. Dallin H. Oaks, mkutano mkuu wa Okt. 1993 (Ensign, Nov. 1993, 75).

  11. Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 38.4.2.8, Gospel Library.

  12. Kitabu cha Maelezo Jumla, 38.4.2, Gospel Library.

  13. Kitabu cha Maelezo Jumla, 38.6.20, Gospel Library.