Vipaji Vilivyofichika
Onyesho la vipaji?
Ee, angalia ni watu wangapi tayari wamejiandikisha! Natamani ningelikuwa na kipaji.
Unamaanisha nini?
“Siwezi kuimba. Mimi siyo mzuri katika mchezo wowote Kamwe siwezi kupata alama nzuri za ufaulu. Mimi siyo mzuri kwa chochote.
Kwa nini siwezi kuwa mkamilifu kwa kila kitu, kama Yesu?!
Unajua, kwa kadiri tunavyojua, Yesu hakucheza dansi au kupiga ala yoyote ya muziki pia.
Hmm, sikuwahi kufikiria hilo. Mbaya zaidi siwezi kuzidisha samaki.
Lakini bado una baadhi ya vipaji vile vile Yeye alivyonavyo.
Yesu Kristo alikuwa rafiki mwema, na wewe ndivyo ulivyo. Ni mojawapo ya vipaji vyako vyenye nguvu.