2025
Wapi Ninaweza Kupata Tumaini Wakati Mtu Ninayempenda Kafariki?
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ya Julai 2025


Wapi Ninaweza Kupata Tumaini Wakati Mtu Ninayempenda Kafariki?

mvulana

Wakati baba yangu alipofariki, kitu kilichonisaidia zaidi kilikuwa imani yangu katika Yesu. Kabla ya familia yangu kujiunga na kanisa, tulikuwa Wakatoliki. Sikupenda kwenda kanisani, lakini mama yangu alikuwa mwaminifu sana. Baada ya baba yangu kufariki, nakumbuka mama yangu akisema hakutaka kuamini tena.

Mama yangu alikuwa na rafiki ambaye alikuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, na aliwaleta wamisionari nyumbani kwetu. Tulikuwa na masomo pamoja na kuanza kwenda kanisani. Nilianza kuamini katika Yesu na Mungu na imani yangu ilianza kukua. Japokuwa baba yangu alikuwa amefariki, nilikuwa na imani kwamba siku moja tutamwona tena. Tunaweza kuishi pamoja mbinguni kwa sababu ya Yesu Kristo.

Yesu Kristo siku zote yupo kwa ajili yako. Unapohisi huzuni au wasiwasi au unapokuwa na siku mbaya, unaweza kumgeukia Yeye kwa sababu Yeye anakupenda. Yeye atapigana kwa ajili yako.

Simone C., umri miaka 18, Vilnius, Lithuania

Hufurahia kucheza mpira wa ndani ya maji, mpira wa wavu, na kinanda cha mkono