Sauti za Vijana
Mtumaini Bwana
Kielelezo na Katelyn Budge
Wakati akina dada wamisionari walipoifundisha familia yangu kwanza kuhusu mpango wa wokovu baada ya baba yangu kufa, wakati mwingine nilipatwa na wasiwasi na sikujua kama niliuamini. Lakini kaka zangu walikuwa watulivu na walinisaidia kuamini na sio kufikiri zaidi kila kitu.
Wakati mwingine sijihisi kuwa imara sana Kanisani. Lakini kama nina kitu fulani nina wasiwasi nacho au tatizo ninalokabiliana nalo, daima ninajaribu kufikiria jambo moja: Mtumaini Bwana. Yeye ananiongoza hadi pale ninapopaswa kuwa.
Hiyo ndiyo sababu ninataka kwenda misheni—ili kumwelewa Yeye zaidi na kuelewa kile Yeye anachotaka mimi nifanye. Ninapowaona wamisionari na roho waliyo nayo pamoja nao, ninataka kuwa kama wao. Wao ni mifano mizuri ya wanafunzi wa Yesu Kristo. Kwa sababu ya mifano yao, ninafurahi sana kwenda misheni baada ya kuhitimu shule ya upili. Ninataka kutoa furaha na maarifa niliyo nayo kwa marafiki zangu na wengine.
Dora C., umri wa miaka 18, Vilnius, Lithuania
Anafurahia mpira wa ndani ya maji na kucheza fidla.