2025
Mungu Daima Yu pamoja Nawe
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ya Julai 2025


Mungu Daima Yu pamoja Nawe

Hata wakati sikuamimi katika Mungu, Yeye bado alinipenda na kunilinda.

msichana akiangalia ajali ya gari

Kielelezo na Uran Duo

Mungu Alinijua Mimi kabla Sijamjua Yeye.

Nilipokuwa na umri wa miaka minane, wamisionari walikutana na bibi yangu na shangazi mtaani. Baada ya kujifunza kuhusu injili, sote tulibatizwa. Mnamo 2020, hata hivyo, ilitubidi tuache kwenda kanisani kwa sababu ya UVIKO. Hatimaye tuliacha kuamini.

Miaka miwili iliyopita, sikuamini hata katika Mungu au kujua kama Yeye ni halisi. Siku moja baada ya shule, nilitaka kuvuka mtaa kununua kitafunwa. Lakini sauti iliniambia nisivuke barabara. Nilisimama, na magari mawili yaligongana mbele yangu. Kama ningevuka mtaa, magari yale yangenigonga au labda yangeniua. Nilijua wakati huo kwamba Mungu alinijua na alinipenda. Ingawa sikuamini katika Yeye na sikuhudhuria kanisa wakati huo, bado Yeye alinipenda na kunilinda.

Nilianza kusoma Kitabu cha Mormoni tena na kujua kwamba ni neno la Mungu. “Nilianza kwenda kanisani pia. Ninapokwenda kanisani, ninahisi amani, upendo wa Mungu na msaada Wake. Ninahisi kwamba Yeye daima yu pamoja nami, na hiyo inanifanya niwe na furaha.

Wimbo wangu ninaoupenda ni “Mimi ni Mtoto wa Mungu” kwa sababu unanikumbusha kwamba Baba wa Mbinguni anatupenda na anatusaidia. Pia ninapenda andiko 2 Nefi 2:27, ambalo linazungumzia jinsi tunavyokuwa huru kuchagua kati ya mema na mabaya.

Mungu Yu pamoja Nami katika Changamoto Zangu

Miezi mingi iliyopita, kaka yangu alianza kuja kanisani pamoja nami, lakini baada ya muda aliacha. Ana wasiwasi kuhusu kile marafiki zake na wengine watakavyomfikiria. Anafikiri kwamba ni aibu kwenda kanisani kwetu, lakini ninamwambia kwamba hatupaswi kujali marafiki wanafikiria nini. Ni kile Mungu anachofikiria ndicho muhimu.

Familia yangu hawaendi kanisani. Mimi huenda peke yangu. Kwa sababu mtaa wangu hauna basi linaloenda kwenye jengo la Kanisa, ninatembea takribani dakika 30 kufika huko. Familia yangu ina wasiwasi watu wengine watafikiria nini juu yao, lakini nasema kwamba hilo siyo muhimu kwa sababu najua ni kweli.

Ninapokutana na marafiki zangu, wakati mwingine wanakunywa kahawa. Na ninapoona hilo, wakati mwingine mimi nataka kunywa kahawa pia. Lakini nakumbuka kwamba Mungu yu pamoja nami. Yeye hushika mkono wangu na kunisaidia. Ninasikia sauti ambayo inaniambia nisifanye hivyo, na ninajua kwamba Mungu ananisaidia kushinda changamoto hizi.

msichana

Ni vigumu kuhudhuria kanisa bila familia yake, lakini Nara anajua kwamba Mungu anampenda na anambariki. Hata alimlinda kutokana na ajali ya gari wakati mmoja.

Ushauri Wangu kwa Wengine Kama Mimi

Kama ningetoa ushauri kwa mtu katika hali yangu, ningewaambia kwamba umebarikiwa sana, na una imani kubwa. Hauko peke yako, kwa sababu waumini wa Kanisa na wamisionari wanaweza kukupa ushauri mzuri. Mungu anakupenda. Wewe ni mwana au binti Yake, na Yeye anataka kukusaidia.

Mwandishi anaishi Yerevan, Armenia.