2025
Nina maamuzi mengi makubwa ya kufanya. Ni kwa jinsi gani ninapata ufunuo binafsi?
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ya Julai 2025


Maswali na Majibu

“Nina maamuzi mengi makubwa ya kufanya. Je, ninapataje ufunuo binafsi?”

msichana

“Jifunze faida na hasara na uchaguzi wa kile kitakachokuweka katika mfungamano na Mungu. Kumbuka kuomba kabla, wakati wa, na baada ya kufanya uamuzi wako. Roho atathibitisha kwako kile kilicho sahihi.”

Laneah S., 16, Utah, Marekani

mvulana

“Kusali na kusoma maandiko kutasaidia asilimia 100. Maandiko yanasema, ‘Ombeni, nanyi mtapewa.’ Basi ombeni! Kisha fanyia kazi kile unachohitaji. Kumbuka, Bwana daima atatoa!”

Parker B., 16, California, Marekani

mvulana

“Mwombe Baba wa Mbinguni na usome maneno Yake. Angalia jinsi Roho Mtakatifu anavyokufikia kwa kuandika misukumo kila siku, na unaweza kupata mpangilio kuhusu jinsi unavyopata ufunuo binafsi.”

Caleb A., 18, Carolina Kaskazini, Marekani

mvulana

“Kitabu cha Mormoni ni mojawapo ya zana bora tulizonazo za kupokea ufunuo binafsi. Tunaweza kujifunza kutokana na mifano ya manabii wa kale.”

João C., 19, São Paulo, Brazili

msichana

“Jibu lako wakati mwingine halitakuja mara moja, na wakati mwingine litatokea. Wakati mwingine jibu huja kama hisia maalumu au wimbo ambao unausikia kanisani. Familia na marafiki wa kuaminika wanaweza pia kutoa ushauri mzuri.”

Anabel V., 12, Utah, Marekani