2025
Kushiriki Injili … katika Bustani ya Burudani?
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ya Julai 2025


Kutumia Mwongozo

Kushiriki Injili … katika Bustani ya Burudani?

Hivi karibuni nilienda kwenye bustani ya burudani pamoja na baadhi ya marafiki kutoka kanisani. Wakati rafiki yangu Evie pamoja nami tuliposimama kwenye mstari kwa ajili ya rolakosta, kijana mmoja aitwaye Erik alianza kuzungumza nasi kuhusu chaneli yake ya YouTube. Aliongea takribani kwa dakika 15 hivi kuhusu jinsi baadhi ya watu shuleni kwake walivyomkejeli na kumwambia afute chaneli yake.

Kanisani, viongozi wetu walikuwa wametupa changamoto ya kuchukua mwongozo wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana na kuushiriki na mtu fulani. Erik alionekana kama alikuwa na matatizo na marafiki, hivyo nilidhani labda mwongozo ungeweza kumsaidia.

Niliutoa na nilimwambia aumiliki. Aliuliza ilikuwa ni nini, na nilielezea kwamba ulikuwa kutoka Kanisani kwangu na kwamba ungeweza kumsaidia kufanya maamuzi mazuri na kumfundisha mambo mengine mazuri. Nilimwambia alipaswa kuusoma wakati anapokuwa na muda. Alisema SAWA, aliuingiza mfukoni mwake, na kuendelea kuzungumza kuhusu chaneli yake ya YouTube.

Sijui kama aliwahi kusoma mwongozo ule, lakini tukio hili lilinifundisha kwamba unaweza kuwa mmisionari katika umri wowote, katika sehemu yoyote—hata katika bustani ya burudani.