Sehemu ya Burudani
Bangili ya Mtegemee Kristo
Je, umewahi kuona bangili kutoka kwenye video ya Dhima ya Vijana kwa mwaka 2025? Unaweza kutengeneza moja kama hiyo!
Angalia mafunzo ili kutengeneza toleo lililorahisishwa la msingi wa bangili. Kisha ni wakati wa kuongeza sehemu muhimu zaidi—jua—ili kukukumbusha kumtegemea Kristo. Ni njia gani za ubunifu ungeweza kuongeza jua kwenye bangili yako? (Fikiria karatasi, uzi, mawe au kitu kingine chochote!)
Tutumie kwa barua pepe picha ya bangili yako iliyokamilika kwa tsoy.ChurchofJesusChrist.org kwa nafasi ya kuionyesha.
Mafunzo ya Bangili
Video ya Dhima ya Vijana
Usipofushwe na Ujanja
Mafundisho na Maagano 76:75 inasema kwamba wale wanaokwenda kwenye ufalme wa terestria (badala ya selestia) “wamepofushwa na ujanja wa wanadamu.” Hapa kuna mchezo wa kufurahisha ambao unaweza kuwa mgumu kuliko unavyoonekana.
Picha hizi tatu za “ujanja” zinaweza kuwa kile kinachoonekana, au zinaweza kuwa udanganyifu wa macho. Je, unaweza kutambua ukweli?
1. Je, mstari huu ni rangi hiyo hiyo katika miisho yote miwili, au rangi tofauti?
Hiyo hiyo
Tofauti
Dokezo: Kunja ukurasa ili mwisho wa mstari uwe karibu na kila mmoja, au kata mstari toka nyuma ili kuangalia.
2. Je, hii ni picha ya msichana, au mwanamke mzee?
msichana
Mwanamke mzee
Dokezo: Angalia kwa karibu. Hili linaweza kuwa swali gumu.
3. Je, mistari ya kijivu imeelekea upande, au imenyooka moja kwa moja hadi mwiso?
Imeelekea upande
Imeyonyooka
Dokezo: Funika vigae vyeusi na vyeupe ili kuangalia.
Kulinganisha Misukosuko
Tafuta kila Nambari 1 (zipo tatu). Chora mstari kutoka kila 1 hadi kwenye Namba 2 inayofanana. Kisha unganisha kila Namba 2 na nambari yake inayofanana na Nambari 3. Mara kila kitu kinapokuwa kimelinganishwa, angalia picha uliyoumba na uamue ufalme gani wa utukufu unawakilishwa.
1. Ufalme wa Selestia
2. Utukufu wa Jua
3. Vitu Vyote Ni Vyao
1. Ufalme wa Terestria
2. Utukufu wa Mwezi
3. Waheshimiwa lakini Wamepofushwa
1. Ufalme wa Telestia
2. Utukufu wa Nyota
3. Alipata Fursa lakini Hakupokea Injili
Picha ya mwisho: Ufalme wa __________________________
Unahitaji dokezo?
Ufalme wa Selestia: Mafundisho na Maagano 76:50–70
Ufalme wa Terestria: Mafundisho na Maagano 76:71–80
Ufalme wa Telestia: Mafundisho na Maagano 76:81–88
Vichekesho
Je, mama yako alitumia maelekezo ya mapishi au mchanganyo wa siri?
Val Chadwick Bagley
Unaonekana mwenye wasiwasi sana kuzungumza kanisani. Je, hii ni mara yako ya kwanza?
Hapana! Nimekuwa na wasiwasi mara nyingi.
Derek L. Smith
Majibu
Usipofushwe na Ujanja: 1. Hiyo hiyo, 2. Zote mbili, 3. Imenyooka
Kulinganisha Misukosuko: 1. Ufalme wa Selestia, 2. Utukufu wa Jua, 3. Vitu Vyote Ni Vyao; 1. Ufalme wa Terestria, 2. Utukufu wa Mwezi, 3. Waheshimiwa lakini Wamepofushwa; 1. Ufalme wa Telestia, 2. Utukufu wa Nyota, 3. Hawakuipokea Injili. PICHA YA MWISHO: Ufalme wa Telestia