2025
Unganika
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ya Julai 2025


Unganika

Flavia C.

19, Buenos Aires, Ajentina

msichana

Picha na Christina Smith

Hivi karibuni nilipoteza mguu wangu kwenye ajali ya gari moshi.

Nilikuwa nimekaa ndani ya treni nilipohisi simu yangu ikitoka mikononi mwangu—ni mtu aliniibia. Bila kufikiria, nilimkimbiza mtu huyo kupitia behewa la treni ambalo halikuwa na milango. Sina hakika kile kilichotokea, lakini ghafla nilikuwa chini ya treni, nikipiga kelele kuomba msaada.

Niliamka hospitalini siku chache baadaye. Niligundua ya kwamba nimepoteza mguu wangu wa kulia. Wakati nikiwa hospitalini, nililia mara nyingi. Lakini familia yangu, marafiki na familia ya Kanisa daima walikuwa pamoja nami, wakinisaidia.

Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo pia walinisaidia. Kabla ya kila upasuaji, daima nilisali kwamba kila kitu kitakuwa sawa na kwamba nisingeweza kuogopa. Kila mara nilipohisi kukosa tumaini, Bwana alikuwa pale.

Ninaendelea kuwa bora na ninajitahidi kusonga mbele kwa msaada wa Mwokozi.