2025
Picha Kubwa Zaidi
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ya Julai 2025


Picha Kubwa Zaidi

Bradley R. Wilcox

Je, umewahi kucheza mchezo wa kwa nini? Unaenda kama ifuatavyo:

Kwa nini niende shuleni? Ili uweze kupata kazi nzuri. Kwa nini nipate kazi nzuri? Ili niweze kuoa au kuolewa na kuwa na watoto. Kwa nini nifanye hivyo? Ili watoto wako waweze kwenda shule.

Kisha mchezo huanza tena upya. Inaonekana haina maana bila ile picha kubwa zaidi. Hicho ndicho tulichobarikiwa kuwa nacho. Unaitwa mpango wa furaha, na unatupatia sisi madhumuni na maana. Hutupatia sababu ambazo ni muhimu hapa na milele. Hicho ndicho toleo hili la jarida la Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana linachohusu.

Katika muktadha wa mpango wa Baba wa Mbinguni—pamoja na Yesu Kristo na Upatanisho Wake hasa vikiwa kitovu chake—utapata hamu na nguvu ya kujiandaa kwa ajili ya siku zijazo. Elimu, ajira, familia na huduma yako katika Kanisa vinaweza kuwa vitu vikuu vya kuvitafuta badala ya kuwa mzigo mkubwa.

Umepata hili kwa sababu Yesu Kristo amekupata wewe!

Kwa upendo,

Bradley R. Wilcox

Mshauri wa Kwanza katika Urais Mkuu wa Wavulana