Sura ya 36
Yesu Anaelezea Mafumbo Matatu
Siku moja Yesu alikuwa akila na kuzungumza na watu ambao wengi waliwadhania kuwa wenye dhambi. Baadhi ya Mafarisayo walimuona.
Luka 15:1–2
Mafarisayo waliamini kwamba watu wema hawapaswi kuzungumza na wenye dhambi. Walidhani kwamba Yesu hakuwa mtu mwema kwa sababu alikuwa akizungumza na wenye dhambi.
Luka 15:2
Mwokozi alitaka kuwasaidia Mafarisayo kuelewa ni kwa nini Yeye alikuwa na wenye dhambi. Aliwaambia mafumbo matatu. La kwanza lilikuwa kuhusu kondoo aliyepotea.
Luka 15:3; Mafundisho ya Nabii Joseph Smith, 277