Hadithi za Maandiko
Fumbo la Kwanza: Kondoo Aliyepotea


Fumbo la Kwanza

Kondoo Aliyepotea

mchungaji na kondoo

Mchungaji mwema alikuwa na kondoo 100. Mmoja wao alikuwa amepotea.

Luka 15:4

mchungaji akimtafuta kondoo aliyepotea

Mchungaji aliwaacha wale kondoo 99 kumtafuta yule mmoja aliyepotea. Alipompata, alikuwa na furaha sana.

Luka 15:4–5

mchungaji amembeba kondoo

Mchungaji alimbeba kondoo kumleta nyumbani. Aliwaita rafiki zake wote na majirani waje na kufurahia pamoja naye. Alikuwa amempata kondoo aliyepotea.

Luka 15:5–6

Yesu amesimama

Yesu Kristo aliwaambia Mafarisayo kile ambacho fumbo lilimaanisha. Alisema kwamba wale wanaotenda dhambi ni kama kondoo aliyepotea.

Luka 15:7

Yesu akinyoosha mkono

Kama vile mchungaji alivyotaka kumuokoa kondoo aliyepotea, Yesu anataka kuwaokoa wale wanaotenda dhambi.

Marko 2:17

Yesu amesimama na mtu

Yesu alisema kwamba hiyo ndiyo sababu alikuwa akizungumza na wenye dhambi.

Mathayo 18:11 (ona rejeo chini ya ukurasa 11c); Marko 2:17

Yesu amesimama pamoja na mwanaume na mwanamke

Na kama vile mchungaji alivyokuwa na furaha alipompata kondoo aliyepotea, Yesu hufurahia pale tunapotubu.

Luka 15:6–7