Sura ya 34
Mvulana mwenye Pepo mchafu
Siku moja mtu alimsihi Mwokozi amsaidie mwanawe. Mvulana alikuwa na pepo mchafu ndani yake. Wanafunzi walikuwa wameshajaribu kumponya mwanawe, lakini hawakuweza.
Marko 9:14–18
Yesu alimwambia mtu yule amlete mwanawe Kwake. Mvulana alipokuja, pepo mchafu lilimfanya aanguke chini.
Marko 9:19–20
Mwokozi aliuliza pepo lilikuwa ndani ya mvulana kwa muda gani. Baba alisema kwamba lilikuwa limekuwa ndani yake tangu alipokuwa mtoto.
Marko 9:21
Yesu alisema angemponya mwanae kama baba angekuwa na imani. Baba alianza kulia. Alisema kwamba alikuwa na imani. Lakini alimsihi Yesu amsaidie awe na imani zaidi.
Marko 9:23–24
Yesu aliliamuru pepo limtoke mvulana na kamwe lisimuingie tena. Pepo lilikasirika. Lilimuumiza mvulana tena. Kisha lilimtii Yesu na kutoka.
Marko 9:25–26
Mvulana alikuwa kimya sana kiasi kwamba watu walisema alikuwa amekufa. Lakini Yesu alichukua mkono wake na kumsaidia kusimama. Mvulana alikuwa ameponywa. Pepo lilikuwa limeondoka.
Marko 9:26–27
Baadaye wanafunzi walimuliza Yesu ni kwa nini hawakuweza kulifanya pepo limtoke mvulana. Yesu aliwaambia kwamba wakati mwingine walihitaji kufunga na kusali ili mtu aweze kuponywa.
Mathayo 17:20–21; Marko 9:28–29