Sura ya 25
Mwanamke Anagusa Mavazi ya Yesu
Mwanamke alikuwa mgonjwa sana kwa miaka 12. Alikuwa ameenda kwa madaktari wengi, lakini hawakuweza kumsaidia.
Marko 5:25–26
Siku moja alimwona Yesu akiwa amezingirwa na watu wengi. Aliamini kwamba angeponywa kwa kugusa tu vazi Lake. Alitembea katikati ya umati na kugusa vazi Lake.
Mathayo 9:20–22; Marko 5:27–28
Aliponywa mara moja. Yesu aligeuka na kuuliza, “Ni nani aliyegusa mavazi yangu?”
Marko 5:29–30
Mwanamke alikuwa na hofu. Alipiga magoti mbele ya Mwokozi na kusema kwamba alikuwa amemgusa. Yesu alimwambia kwamba imani yake Kwake ilimponya.
Marko 5:33–34