Sura ya 41
Yesu Anawabariki Watoto
Yesu alikuwa akienda Yerusalemu. Njiani baadhi ya watu walimtaka Yesu awabariki watoto wao. Wanafunzi waliwaambia watu wasimsumbue Yesu.
Marko 10:13
Lakini Yesu Kristo anawapenda watoto. Aliwaambia wanafunzi wawaache watoto waje Kwake. Yesu pia aliwaambia wanafunzi kwamba wanapaswa kuwa kama watoto wadogo. Kisha wataweza kuishi pamoja na Mungu mbinguni.
Marko 10:14–15