Sura ya 8
Mfalme Herode Mwovu
Mamajusi walikuwa wamemwambia Herode kwamba Yesu angekuwa mfalme. Herode alitaka kuwa mfalme pekee. Aliwaambia askari wake wawaue watoto wote katika Bethlehemu na viunga vyake.
Mathayo 2:3, 13, 16
Malaika alimwambia Yusufu awachukue Mariamu na Yesu hadi Misri, nchi iliyokuwa mbali na Bethlehemu. Herode asingemtafuta Yesu huko.
Mathayo 2:13
Yusufu alitii. Yeye na Mariamu na Yesu walikuwa Misri wakati askari wa Herode walipowaua watoto wote katika Bethlehemu na viunga vyake.
Mathayo 2:14, 16
Baada ya Mfalme Herode kufa, malaika alimwambia Yusufu awapeleke Yesu na Mariamu nyumbani. Yusufu aliwapeleka Nazareti, ambapo Yesu alikuwa salama.
Mathayo 2:19–21, 23