Sura ya 31
Yesu Anamponya Kiziwi
Watu fulani walimleta mtu kwa Yesu. Mtu huyo alikuwa kiziwi na hakuweza kuzungumza vizuri. Watu walimtaka Mwokozi amponye.
Marko 7:32
Yesu alimwongoza mtu huyo mbali na wengine. Aliweka vidole vyake katika masikio ya mtu huyo. Aligusa ulimi wa mtu huyo na kumbariki.
Marko 7:33–34
Sasa mtu huyo angeweza kusikia na kuzungumza. Watu wangeweza kumwelewa. Yesu aliwasihi watu wasimwambie yeyote kile kilichotokea, lakini watu walimwambia kila mtu.
Marko 7:35–36