Sura ya 9
Mvulana Yesu
Yesu alilelewa katika mji wa Nazareti. Alijifunza mambo mengi na “akaongezeka nguvu, … na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.”
Luka 2:39–40
Yesu alipokuwa na miaka 12, Alienda na Yusufu na Mariamu katika kikundi cha watu kwenye sherehe Yerusalemu. Walikuwa huko kwa siku kadhaa.
Luka 2:41–43
Wakati Yusufu na Mariamu walipoondoka kwenda nyumbani, walifikiria kwamba Yesu alikuwa akitembea kurudi Nazareti pamoja na rafiki Zake. Lakini Yesu alikuwa amebaki Yerusalemu.
Luka 2:43–44
Wakati Yusufu na Mariamu walipomtafuta Yesu, hawakuweza kumpata. Hakuna yeyote katika kikundi chao aliyekuwa Amemwona. Hivyo Yusufu na Mariamu walirudi Yerusalemu. Walimtafuta Yesu kwa siku tatu. Walihuzunika sana.
Luka 2:44–46
Hatimaye walimpata Yesu Hekaluni, akizungumza na baadhi ya walimu. Alikuwa akijibu maswali yao. Walimu walishangazwa na mengi ambayo Yesu aliyajua.
Luka 2:46–47 (ona rejeo chini ya ukurasa 46c)
Mariamu alimwambia Yesu kwamba yeye na Yusufu walikuwa na hofu kumhusu Yeye. Yesu alijibu kwamba alikuwa akifanya kazi ya Baba Yake — kazi ya Mungu. Yusufu na Mariamu hawakuelewa.
Luka 2:48–50
Yesu alienda nyumbani Nazareti pamoja na Yusufu na Mariamu na kuwatii.
Luka 2:51
Yesu alijifunza zaidi na zaidi kuhusu kazi ya Baba Yake wa Mbinguni.
Luka 2:52
Alikuwa mrefu na mwenye nguvu.
Luka 2:52
Watu walimpenda. Alifanya kile Mungu alimtaka Yeye afanye.
Luka 2:52
Mungu Alimpenda.
Luka 2:52