Sura ya 32
Petro Anashuhudia juu ya Kristo
Yesu aliwauliza wanafunzi Wake watu walidhani Yeye ni nani.
Mathayo 16:13; Marko 8:27; Luka 9:18
Wanafunzi walijibu kwamba baadhi ya watu walidhani Yesu alikuwa Yohana Mbatizaji. Wengine walidhani alikuwa nabii wa Agano la Kale aliyekuwa amefufuka.
Mathayo 16:14; Marko 8:28; Luka 9:19
Yesu aliwauliza wanafunzi Wake walidhani Yeye alikuwa ni nani. Petro alisema, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”
Mathayo 16:15–16; Marko 8:29; Luka 9:20
Yesu alieleza kwamba ushuhuda wa Petro haukuja kutoka kwa mafundisho ya watu. Ushuhuda wake ulikuwa umekuja kwa ufunuo kutoka kwa Mungu.
Mathayo 16:17
Yesu alimwahidi Petro kwamba angempa ukuhani na mamlaka ya kuongoza Kanisa Lake. Kisha Petro na wanafunzi wangekuwa na mamlaka ya kuanzisha Kanisa la Yesu duniani.
Mathayo 16:18–19
Yesu aliwaambia wanafunzi Wake wasimwabie yeyote kwanza kwamba Yeye alikuwa ndiye Kristo. Kwanza alihitaji kuteseka, kuuwawa, na kufufuka siku ya tatu.
Mathayo 16:20; Marko 8:30–31; Luka 9:21–22