141
Bwana, Nyumba Yako
Kwa unyenyekevu
1. Bwana, nyumba yako
Twaipenda sana;
Furaha inayo
Isiyopimika.
2. Ni nyumba ya sala.
Hukutana watu,
Nawe upo Bwana
Wote kusalimu.
3. Injili twapenda
Yaleta amani
Ya kufurahisha,
Ya kutufariji.
Maandishi: William Bullock, 1797–1874
Muziki: Leroy J. Robertson, 1896–1971. © 1948 IRI
Zaburi 26:8