94
Ee Baba wa Milele
Kwa unyenyekevu
1. Ee Baba wa milele,
Uliye mbinguni,
Katika jina Lake,
Takasa, bariki—
Ikiwa tu wasafi—
Mkate, divai,
Ili tuikumbuke
Damu nao mwili.
2. Dhabihu takatifu
Tusiyoelewa,
Kusamehewa dhambi,
Na kumkumbuka,
Ili tushuhudie
Kuteswa kwa Kristo,
Tuwe na Roho wake,
Na upatanisho.
3. Na Yesu, Mteule,
Akashuka chini
Kujitoa dhabihu
Kuokoa nafsi—
Asiye na mvuto,
Wa kutamaniwa—
Mwokozi wa ahadi
Akatutakasa.
4. Ile hekima kuu,
Mpango kamili
Ulifanya wokovu,
Neno kuwa mwili,
Kushuka duniani
Awe mwanadamu,
Afe, japo Mfalme,
Kutuweka huru.
Maandishi: William W. Phelps, 1792–1872. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.
Muziki: Felix Mendelssohn, 1809–1847
Mafundisho na Maagano 20:77, 79
Isaya 53:2–5