22
Acha Sayuni Ing’are
Kwa ujasiri
1. Acha Sayuni ing’are;
Nuruye yawaka.
Ajapo Mfalme wake,
Mbingu atagawa,
Kote lienee neno
Kuandaa watu
Kukutana na Henoko
Naye Bwana juu.
2. Parapanda pulizeni
Malaika wote.
Taarifa sambazeni
Duniani kote:
Kwamba Yesu kwenye mbingu,
Aja kuokoa
Walio Watakatifu,
Mwovu kuondoa.
3. Litaanza pumziko
Lililotangazwa,
Watakatifu na Kristo
Wataitawala
Milenia duniani;
Bwana, niandae
Nikae nawe Sayuni
Tusitenganishwe.
Maandishi: Edward Partridge, 1793–1840. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.
Muziki: Hajulikani, Württemberg, Germany, mnamo 1784