52
Mwokozi, Niongoze
Kwa sala
1. Mwokozi, niongoze
Dhoruba niipite;
Mawimbi yanizonga,
Hatari zajificha.
Mwenye ramani zote,
Mwokozi, niongoze.
2. Kama mwana kwa mama,
Bahari watuliza;
Mawimbi yakutii
Usemapo “Amani!”
Nahodha na Mfalme,
Mwokozi, niongoze.
3. Niifikapo pwani,
Kufura kwa mawimbi
Kwatisha pumziko;
Naegamia kwako,
Nasikia wasema,
“Tulia; Naongoza.”
Maandishi: Edward Hopper, 1818–1888
Muziki: John Edgar Gould, 1822–1875
Marko 4:39–41
Zaburi 48:14