74
Sala Tamu
Kwa sala
1. Sala tamu! Sala tamu!
Yanirudisha kwa Mungu
Nakuwa mbele ya enzi,
Nikaseme mahitaji.
Ninpopatwa na shida,
Nafsi hupata faraja
Na kuyakwepa maovu,
Irudipo sala tamu!
Na kuyakwepa maovu,
Irudipo sala tamu!
2. Sala tamu! Sala tamu!
Napeleka dua zangu
Kwake aliye mkweli
Nafsi yangu abariki.
Nitafute uso wake,
Na nishike neno lake,
Nimpe mzigo wangu
Ikifika sala tamu!
Nimpe mzigo wangu
Ikifika sala tamu!
Maandishi: Yanahusishwa na William W. Walford, 1772–1850, yamebadilishwa
Muziki: William B. Bradbury, 1816–1868, umebadilishwa
Zaburi 55:16–17, 22
Wafilipi 4:6–7