147
Tupo Waaminifu wa Imani
Kwa shauku
1. Eti! Vijana wasite
Haki kuitetea?
Huku asumbua mwovu,
Tuache kupambana? La!
[Chorus]
Tupo waaminifu wa imani
Ya wazazi wetu na ya Nabii;
Na kwa Mungu,
Watiifu,
Daima tu waadilifu.
2. Twajua nguvu za giza
Zinampinga Kristo,
Je, watoto wa ahadi
Hawatashika neno? La!
[Chorus]
Tupo waaminifu wa imani
Ya wazazi wetu na ya Nabii;
Na kwa Mungu,
Watiifu,
Daima tu waadilifu.
3. Tutatafuta wokovu;
Ukweli tutashika;
Tutasali tuwe macho
Kwa ari ya ujana. Na’m!
[Chorus]
Tupo waaminifu wa imani
Ya wazazi wetu na ya Nabii;
Na kwa Mungu,
Watiifu,
Daima tu waadilifu.
4. Twapania kustahili
Ufalme wake Kristo,
Na waaminifu wote
Waliotii neno. Na’m!
[Chorus]
Tupo waaminifu wa imani
Ya wazazi wetu na ya Nabii;
Na kwa Mungu,
Watiifu,
Daima tu waadilifu.
Maandishi na muziki: Evan Stephens, 1854–1930
1 Timotheo 4:12