85
Roho Wako Katugusa
Kwa hamasa
1. Roho wako katugusa,
Na kwa ushawishi wake
Tunapata dira upya,
Twahisi ukaribuwe.
Hata kichaka cha moto
Hakigusi kama Roho.
2. Je! Nyoyo hazikuwaka?
Twajua Roho yu nasi.
Anafanya kutumika;
Anafanya njia wazi.
Tushawishi kila siku,
Bwana, kwenye kila kitu.
Maandishi: Frank I. Kooyman, 1880–1963. © 1948 IRI
Muziki: Alexander Schreiner, 1901–1987. © 1948 IRI
Luka 24:32 (13–35)