27
Bwana Ni Mwokozi
Kwa shauku
1. Bwana ni Mwokozi
Na Mfalme wenu!
Mshangilieni
Na kumuabudu.
[Chorus]
Msifuni! Shangilia
Mkiimba kwa furaha!
Msifuni! Shangilia
Mkiimba kwa furaha!
2. Kitini pa enzi,
Bwana atawala.
Mungu wa ukweli
Alituokoa.
[Chorus]
Msifuni! Shangilia
Mkiimba kwa furaha!
Msifuni! Shangilia
Mkiimba kwa furaha!
3. Alishinda Kristo
Kote kutawala,
Funguo za kifo
Bwana alipewa.
[Chorus]
Msifuni! Shangilia
Mkiimba kwa furaha!
Msifuni! Shangilia
Mkiimba kwa furaha!
Maandishi: Charles Wesley, 1707–1788
Muziki: Horatio Parker, 1863–1919
Wafilipi 4:4
Zaburi 32:11