176
Familia Huwa za Milele
Kwa uchangamfu
1. Nina familia yangu.
Na kwangu ni wema.
Nataka niishi nao milele daima.
[Chorus]
Familia huwa za milele
Kwa mpango wa Baba.
Niwe na familia yangu daima
Na Bwana amenionesha,
Amenionesha njia.
2. Nikiwa bado mdogo,
Vyema nijiandae,
Nikafunge hekaluni ndoa ya milele.
[Chorus]
Familia huwa za milele
Kwa mpango wa Baba.
Niwe na familia yangu daima
Na Bwana amenionesha,
Amenionesha njia.
Maandishi: Ruth M. Gardner, 1927–1999. © 1980 IRI
Muziki: Vanja Y. Watkins, kuz. 1938. © 1980 IRI