90
Twapokea Sakramenti
Kwa kuabudu
1. Twapokea sakramenti,
Twakugeukia,
Ewe Mwana wake Mungu,
Uliyetufia.
Neema isiyokoma,
Nao upendowe,
Umetupa na uzima
Wa milele yote.
2. Kumbukumbu twarejesha
Kuzitubu dhambi;
Njia ni utakatifu—
Ndivyo uliishi.
Msamaha ni zawadi
Tunayotafuta.
Kwa mikono ya ahadi,
Sakramenti twala.
3. Tunakusifu na wimbo,
Tunakuabudu.
Zitabaki mioyoni
Baraka za siku.
Tupatie ujasiri
Wa kusikiliza.
Ee Bwana tunashukuru;
Tutakufuata.
Maandishi: Lee Tom Perry, 1951–2011. © 1985 IRI
Muziki: Daniel Lyman Carter, kuz. 1955. © 1985 IRI