44
Enyi Wenye Shukrani
Kwa shauku
1. Enyi wenye shukrani;
Mavuno imbieni.
Ndani yamekusanywa;
Baridi imeanza.
Vyote atoa Mungu
Kwa uhitaji wetu.
Njooni hekaluni
Mavuno imbieni.
2. Dunia ni ya Mungu,
Ni shamba la kusifu:
Magugu kwa majuto,
Bali shangwe kwa ngano.
Kwanza jani na suke,
Halafu mbegu yote.
Bwana amekubali
Tuwe mbegu halisi.
Maandishi: Henry Alford, 1810–1871
Muziki: George J. Elvey, 1816–1893
Marko 4:26–28