56
Bwana Wetu, Upendo Wake Wang’ara
Kwa unyenyekevu
1. Bwana wetu,
Upendo wake wang’ara
Kama nuru
na miale yake.
Hushawishi,
Turudi tena kwa Baba,
Kushiriki
Utukufu wake.
2. Roho mwema,
Hunong’oneza moyoni
Yale mema,
Kumzidi pepo.
Isikike
Sauti ya tumaini,
Itufunge
Kwake kwa upendo.
3. Baba, Mungu,
Sikia yetu maombi,
Ni ajabu
Dhabihu ya Mwana.
Asifiwe.
Amri zako tutatii.
Ee Mfalme,
Twakufurahia.
Maandishi: Edward L. Hart, 1916–2008. © 1977 IRI
Muziki: Crawford Gates, 1921–2018. © 1977 IRI
Yohana 15:12–14