9.
Wewe umebarikiwa kwa funguo na mamlaka ya ukuhani
Mathayo 16:18–19
Wakati Yesu alipomfundisha Petro kuhusu mamlaka ya ukuhani, Yeye alizungumzia juu ya funguo. Funguo hutumika kufunga na kufungua vitu. Funguo za ukuhani zinaweza kufungua nguvu za Mungu, vipawa, na baraka katika maisha yako.
Kweli za Milele
Funguo zote za ukuhani na mamlaka huja kupitia Yesu Kristo. Kila mwenye ukuhani anaweza kutafuta asili ya mamlaka yake kwa kurudi nyuma hadi Kwake. Mwokozi anaamua nani anapokea mamlaka haya na nani anapokea funguo za ukuhani. Tunaamini ufahamu Wake mkamilifu.
Yesu Kristo amerejesha ukuhani Wake katika siku yetu. Yeye anaelekeza jinsi ukuhani utakavyotumika. Adamu, Musa, Petro, na manabii wengine wengi kote katika historia walipokea funguo za ukuhani. Katika siku yetu, Joseph Smith alipokea funguo za ukuhani kutoka kwa Yohana Mbatizaji, Petro, Musa, Elia, Eliya, na wengineo. Washiriki wa Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wanashikilia funguo hizi zote za ukuhani leo. Viongozi wa ukuhani wa eneo husika na marais wa akidi pia wanashikilia funguo za ukuhani kwa ajili ya miito yao. Funguo za ukuhani zinatawala kazi ya Mungu. Zinawapa mamlaka na kuwawezesha wanaume na wanawake kusaidia katika kazi hiyo.
Mamlaka ya ukuhani huwabariki watoto wote wa Mungu. Kwa sababu ukuhani ulirejeshwa, unaweza kupokea ibada na kufanya maagano na Mungu. Unaweza kutenda katika jina la Mungu unapopokea jukumu au wito kutoka kwa mtu mwenye mamlaka.
Mialiko
Kubali miito ya Kanisa na hudumu kwa uaminifu. Unapopokea wito wa Kanisa, unasimikwa kwa mamlaka kutoka kwa Mungu kuhudumu katika jukumu hilo. Unaweza pia kupokea mwongozo kutoka kwa Mungu kwa ajili ya huduma yako. Unapohudumu, unamwakilisha Yesu Kristo. Mpe Yeye uwezo wako wote.
Wakubali wale ambao Mungu amewaita kuhudumu. Kuwakubali kunamaanisha zaidi ya kuinua mkono wako wakati jina linaposomwa katika mkutano wa Kanisa. Inamaanisha kuunga mkono na kusaidia. Tafuta njia za kuonyesha kwamba unawakubali watu ambao Yesu Kristo amewaita kuhudumu katika Kanisa Lake.
Timiza majukumu kutoka kwa viongozi wako wa Kanisa—ikijumuisha kutoka kwa urais wa akidi yako au wa darasa. Wana mamlaka kutoka kwa Mungu, ambayo wanayanaibisha kwako kwa ajili ya jukumu hilo. Unaweza kupangiwa kumtumikia mtu fulani, kuwakaribisha watu wanapowasili kwenye mkutano wa sakramenti, au kusaidia katika shughuli. Jukumu lolote lile, lione kama fursa ya kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo na wahudumie watoto wa Mungu.
Baraka Zilizoahidiwa
Unaweza kuamini kwamba ibada unazopokea zimeidhinishwa na Yesu Kristo. Hii ni mojawapo ya mambo ambayo hufanya Kanisa la Yesu Kristo kuwa la kipekee. Kupitia ibada za ukuhani, nguvu za Mungu hujidhihirisha.
Utakuwa chombo katika mikono ya Bwana Unapomhudumia Bwana kwa mamlaka Yake na chini ya maelekezo ya watumishi Wake wenye kushikilia funguo za ukuhani, Yeye atakusaidia kujua jinsi ya kuwatumikia wengine katika kazi Yake. Yesu Kristo ni nguvu yako. Huduma yako itakusaidia kusogea karibu zaidi na Yeye na kukuletea shangwe.
Maswali na Majibu
Nani katika kata yangu anashikilia funguo za ukuhani? Askofu na marais wa akidi za wazee, walimu, na akidi za mashemasi wanashikilia funguo za ukuhani. Hii inamaanisha Bwana amewapangia kuelekeza jinsi ukuhani unavyotumika kuhudumu na kumbariki kila mtu katika kata.
Ni kwa jinsi gani funguo za ukuhani zinanibariki mimi? Ibada kama ubatizo na sakramenti zinaruhusiwa kwa funguo za ukuhani. Unapopokea wito kanisani, unasimikwa chini ya maelekezo ya mtu anayeshikilia funguo. Hii inakubariki wewe kwa mamlaka ili kuhudumu katika wito huo. Viongozi wa Kanisa na walimu wanaokuhudumia pia walipokea mamlaka ya ukuhani kupitia funguo.
Ni kwa jinsi gani wanaume na wanawake wanahudumu kwa mamlaka ya ukuhani? Wanaume wanaostahili wametunukiwa ukuhani juu yao na kutawazwa katika ofisi za ukuhani kama shemasi, mwalimu, kuhani, na mzee. Wote, wanawake na wanaume ambao wamesimikwa kuhudumu katika wito wanapokea mamlaka ya ukuhani yaliyonaibishwa kutoka kwa Mungu ili kutimiza wito huo. Vivyo hivyo ni kweli kwa wanawake na wanaume wanaopokea jukumu kutoka kwa kiongozi wa Kanisa.
Ona Mafundisho na Maagano 35:24–27 (Kanisa linaongozwa na funguo ambazo Bwana ametoa); 107:18–20 (funguo za Ukuhani wa Melkizedeki na Ukuhani wa Haruni); 110:11–16 (Musa, Elia, na Eliya walirejesha funguo).
Maswali ya Kibali cha Hekaluni
-
Je, unamkubali Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kama nabii, mwonaji na mfunuzi na kama mtu pekee duniani aliyepewa mamlaka ya kutumia funguo zote za ukuhani?
-
Je, unawakubali washiriki wa Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji na wafunuzi?
-
Je, unawakubali Viongozi Wakuu wengine wenye Mamlaka na viongozi wa Kanisa wa eneo lako?