Vijana
Fanya chaguzi zenye mwongozo wa kiungu


Fanya chaguzi zenye mwongozo wa kiungu

Ndani ya Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana, utapata mafundisho ya Yesu Kristo na ya manabii Wake. Ukiwa na kweli hizi kama mwongozo wako, unaweza kufanya chaguzi zenye mwongozo wa kiungu ambazo zitakubariki sasa na milele yote.

Wewe ni mtoto mpendwa wa kiroho wa Mungu. Mpango Wake mkuu wa furaha unafanya iwezekane kwa wewe kukua kiroho na kukuza uwezekano wako wa kiungu. Yeye alimtuma Yesu Kristo kuwa Mwokozi wako.

Baba yako wa Mbinguni anakutumainia wewe. Amekupa baraka kuu, ikijumuisha utimilifu wa injili na ibada takatifu na maagano ambayo yanakuunganisha wewe Kwake na kuleta nguvu Yake ndani ya maisha yako. Pamoja na maagano haya huja shangwe na majukumu yaliyoongezwa. Anajua unaweza kuleta utofauti katika ulimwengu na hiyo inahitaji, katika hali nyingi, kuwa tofauti na ulimwengu. Tafuta mwongozo wa Baba yako wa Mbinguni pale unapofanya chaguzi. Yeye atakubariki kwa mwongozo wa kiungu kupitia Roho Mtakatifu.

Yesu Kristo ndiye njia ya kwenda kwenye shangwe ya milele. Kadiri unavyotumia uhuru wako wa kuchagua kumfuata Yesu Kristo, unakuwa kwenye njia ambayo inaongoza kwenye furaha ya milele. Mfanye Yesu Kristo awe kiwango chako, msingi wako imara wa mwamba. Jenga maisha yako juu ya mafundisho Yake, na pima chaguzi zako kwa mafundisho hayo. Maagano unayofanya unapobatizwa, wakati wa sakramenti na hekaluni ni matofali ya kujengea msingi wako imara katika Kristo. Bado utakabiliana na mapambano na vishawishi, lakini Baba wa Mbinguni na Mwokozi watakusaidia kuyapita yote.

Dhumuni la Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana si kukupa jibu la “ndiyo” au “hapana” kuhusu kila uwezekano wa uchaguzi unaoweza kukabiliana nao. Badala yake, Bwana anakualika kuishi katika njia ya juu na takatifu zaidi—maisha yaliyofokasi kwenye kweli za milele na baraka zilizoahidiwa na Bwana. Hii ni njia Yake. Mwongozo huu utakufundisha kuhusu njia Yake. Unaelezea kweli ambazo Yeye amezifunua. Fanya kweli hizi ziwe mwongozo wako wa kufanya chaguzi—chaguzi kubwa, kama vile kufanya maagano hekaluni na kuhudumu misioni, vile vile chaguzi za kila siku, kama vile jinsi ya kuwatendea watu au jinsi ya kutumia muda wako.

Wakati wengine wanaweza kukusaidia, ukuaji wako wa kiroho ni wako binafsi. Ni wajibu wako. Fanya kwa uwezo wako wote ili kufanya vizuri zaidi kila siku, shika amri za Mungu na heshimu maagano yako na wasaidie wengine kuja karibu zaidi na Mwokozi.

Ona Mosia 4:29–30 (njia za kutenda dhambi hazihesabiki, hivyo lazima tujichunge wenyewe); Helamani 5:12 (jenga msingi wako juu ya Kristo); Mafundisho na Maagano 45:57 (mchukue Roho Mtakatifu kuwa kiongozi wako); 25:13 (yashikilie maagano yako).

Jinsi mwongozo huu ulivyopangiliwa

Kila mada ina sehemu tatu:

  1. Kweli za milele, au mafundisho ya injili iliyorejeshwa ya Yesu Kristo

  2. Mialiko ya kutenda juu ya kweli hizo

  3. Baraka zilizoahidiwa ambazo Bwana anatoa kwa wale wanaoyaishi mafundisho Yake