Ujumbe kutoka kwa Urais wa Kwanza
Wapendwa wetu akina kaka na akina dada vijana,
Tunawapenda, na tuna imani kubwa nanyi. Ninyi kwa hakika ni miongoni mwa roho wateule wa Baba wa Mbinguni, walioletwa duniani wakati huu kufanya mambo muhimu.
Mna nguvu na uwezo zaidi kuliko mnavyoweza kutambua. Na mnapomtegemea Mwokozi, nguvu zenu zinakua na hata kuwa imara zaidi. Yeye ni “nguvu kwa vijana.”
Mwongozo huu utakusaidieni kujenga msingi thabiti kwa ajili ya kufanya chaguzi ili kubaki kwenye njia ambayo inaongoza kwenye uzima wa milele. Utawasaidia kujiandaa kufanya maagano matakatifu hekaluni, kujiandaa kuhudumu misioni na kupata shangwe katika kumfuata Yesu Kristo katika maisha yenu yote. Mna nafasi muhimu katika Kanisa Lake. Yesu Kristo atawasaidia kutimiza makusudi Yake kwa ajili yenu.
Tunajua Mungu yu hai. Ni sala yetu kwamba mtabaki imara kwenye njia ya agano—njia ya kufanya na kushika maagano matakatifu na Mungu. Hiyo ndiyo njia inayoongoza kurudi kwa Baba yenu wa Mbinguni. Mnapofanya hivi, mtakuwa ushawishi kwa mema, kushiriki injili kwa shangwe, kuwakusanya watoto wa Mungu, na kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi. Kumbukeni: Yesu Kristo ni nguvu yenu!
Urais wa Kwanza