Liahona
Je, Mwokozi Mkamilifu Anaweza Kuelewa Jinsi Ilivyo katika Kupambano?
Machi 2026 Liahona


“Je, Mwokozi Mkamilifu Anaweza Kuelewa Jinsi Ilivyo katika Kupambana?,” Liahona, Machi 2026.

Kutoka VW Kila Wiki

Je, Mwokozi Mkamilifu Anaelewa Jinsi Ilivyo katika Kupambana?

Kwa sababu Yesu Kristo ni mkamilifu, wakati mwingine tunasahau kwamba Yeye anajua jinsi ilivyo katika kupambana.

kielelezo cha Yesu Kristo

Kielelezo na Brandon Gonzales

Mimi huwa nafikiri sihusiki na usaidizi wa kiungu wa Kristo ninapokuwa na wakati mgumu. Wakati mwingine ninafikiri kwamba Yeye, Mwokozi asiye na dhambi na mkamilifu, hangeweza kamwe kuelewa jinsi ilivyo katika kupambana.

Nakumbuka kuhisi hivyo hususani kama mmisionari. Ilichukuwa jitihada kubwa kwangu kutambua kwamba Kristo anajua jinsi ilivyo kuwa na wakati mgumu.

Ni kwa jinsi gani angeweza kujua jinsi nilivyojisikia?

Nilidhani nilikuwa kileleni mwa misheni yangu—nilikuwa nikimfundisha mmisionari mpya, nikijiandaa na ubatizo, na kila kitu cha umisionari. Nilihisi furaha sana.

Lakini sikutambua msongo wa mawazo na wasiwasi ukijenga ndani yangu.

Nilikuwa nimejilaza nilale usingizi usiku mmoja nilipoanza kuzunguka katika muda wa kushikwa na hofu ya shambulio la pili ambalo sikuwahi kuwa nayo katika maisha yangu yote—la kwanza likiwa limetokea miaka tisa iliyopita. Miaka tisa!

Kwa nini, baada ya kipindi kidogo tu cha wasiwasi kama mtoto, je, ghafla lilikuwa likijitokeza tena sasa?

Kwa kiburi nilijaribu kuendelea na misheni yangu kama kawaida, nikifikiri ningeweza kutatua matatizo yangu mwenyewe.

Wakati nikipigana mieleka na afya yangu ya akili, mtu fulani alishiriki nami umaizi waliokuwa nao wakati akisoma kuhusu uzoefu wa Mwokozi katika Gethsemane.

Yesu alisema, “Roho yangu ina huzuni nyingi, kiasi cha kufa.” Na kisha Mwokozi alisali, “ Ee Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke: walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe” (Mathayo 26:38–39).

Je, umewahi kuhisi uzito wa huzuni yako mwenyewe? Je, umewahi kumwomba Mungu, “Kuna njia nyingine?”

Kwa utayari mkamilifu, utiifu kamili, na upendo kamili, Mkombozi wetu alikubali mapenzi ya Baba. Alikuwa mkamilifu kwa sababu hakuwa na dhambi, lakini bado alihisi maumivu, huzuni, na upweke.

Hata hivyo, Yeye alishuka chini ya vitu vyote—ili Yeye aweze kutuinua juu.

Rais Jeffrey R. Holland, Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, alifundisha, “Yesu alikuwa mtu wa huzuni’ [Isaya 53:3], maandiko yanasema. Alipitia huzuni, uchovu, kuvunjika moyo na upweke wa hali ya juu. Katika nyakati hizi na nyakati zote, upendo wa Yesu haukushindwa, na wala wa Baba Yake.”

Kristo Anajua kwa Usahihi Jinsi Tunavyojisikia.

Kwa kujua kwamba Kristo alikumbana na mambo magumu kuna nikumbusha kwamba Anaelewa maumivu ya moyo, msongo wa mawazo, uchovu, kukata tamaa, wasiwasi, na upweke zaidi kuliko mtu ye yote.

Alikuwa Yeye aliyelia wakati wa kifo cha Lazaro (ona Yohana 11:33–36). Na ilikuwa Yeye aliyeuliza anilipokuwa anakufa pale msalabani, “Mungu wangu Mungu wangu, mbona umeniacha?” (Marko 3:34).

Lakini Yesu Kristo pia anajua shangwe, upendo, huruma, rehema, na amani kuliko mtu yeyote. Kwa sababu Yeye ni mkamilifu. Hivyo, Yeye anajua kikamilifu jinsi tunavyojisikia.

Rais Holland alishuhudia: “Mojawapo ya faraja kuu ya kipindi hiki cha Pasaka ni kwamba kwa sababu Yesu alitembea njia hiyo ndefu ya upweke kabisa peke yake, sisi hatuhitaji kufanya hivyo. Safari yake ya upweke ilileta ushirika mkubwa kwa ajili ya toleo letu dogo la njia hiyo—utunzaji wa rehema wa Baba yetu wa Mbinguni, wenza usioshindwa wa Mwana huyu Mpendwa, kipawa kikamilifu cha Roho Mtakatifu.”

Nikitambua kwamba Yesu Kristo alielewa kikamilifu kile nilichokuwa nahisi nilipokuwa nahangaika na wasiwasi, mwishowe nilimruhusu anisaidie kubeba mizigo yangu.

Wasiwasi wangu haukuondoka ghafla. Bado nilikuwa na siku ngumu. Kuwa karibu na Kristo kulinipa shangwe ya kudumu katika njia yo yote kwa sababu nilijua Alikuwa hapo pamoja nami, akisema, “Ninajua. Ninajua kikamilifu jinsi unavyojisikia.”

Wakati wa uzoefu huu, Kristo akawa mtu wa karibu zaidi kwangu kumwamini.

Nafikiri kwamba wakati mwingine tunakuwa katika hatari ya kufikiria kwamba ukamilifu wa Kristo unamaanisha kwamba Yeye yuko mbali sana na hafikiki, kwamba matendo Yake makuu na maisha yake ya kimiujiza yanamfanya aonekane kuwa mbali sana na sisi viumbe wa kawaida, tusio wakamilifu, wenye kiburi. Lakini yeye kamwe hajawahi kuwa karibu zaidi nasi kuliko wakati tunapokabiliana na vita vyetu vigumu, huzuni yetu mbaya zaidi, na mapambano yetu ya kuhuzunisha zaidi.

Msimu huu wa Pasaka, tunaweza kukumbuka kwamba Yesu Kristo anajua kwa uhakika jinsi ilivyo kupambana kwa sababu Alikuwa mkamilifu—mtu pekee ambaye angeweza kuhisi maumivu yetu na kubeba mizigo yetu.

Kwa hiyo, unapohangaika, mgeukie Yeye. Yeye anakuelewa kikamilifu