Liahona
Pasaka ya Zamani na Pasaka ya Sasa
Machi 2026 Liahona


Pasaka ya Kale na Pasaka ya Leo

Ona jinsi vipengele vya Pasaka ya Kale vinavyoweza kutuelekeza kwenye dhabihu ya upatanisho ya Yesu Kristo na maagano yetu na Mungu.

Pasaka ya kale inaadhimisha ukombozi wa Bwana ya kuwakomboa watu wa Israeli kutokana na tauni ya mwisho ya kuangamiza misri. Kupitia Musa, Bwana aliwaambia wafanye matendo maalumu ili kwamba malaika mwangamizaji aweze kuwapita na kumwacha mzaliwa wao wa kwanza. Bwana kisha akawakomboa kutoka utumwani na kuwapeleka katika nchi ya ahadi. (Ona Kutoka 12.)

Vipengele mbalimbali vya Pasaka ya Kale vinawakilisha dhabihu ya Yesu Kristo ya kulipia dhambi zetu, vile vile maagano yetu na Mungu.

Mwanakondoo

Mwanakondoo

Mwanakondoo mume mwenye umri wa mwaka mmoja bila mawaa.

Aliuawa na kisha kuokwa kwa moto, mzima—hakuna mifupa iliyovunjika na kichwa, miguu, na sehemu za ndani za kuliwa zimeambatanishwa. Ilikuwa iliwe wakati wa usiku wa Pasaka, hakuna kinachobakia asubuhi. Kama chochote kingebaki, kilipaswa kuunguzwa moto.

Maana yamkini: Yesu Kristo kama dhabihu isiyo na dhambi kwa ajili ya dhambi; utamu wa kuja Kwake ulitofautiana na uchungu wa dhambi; Kujitolea kwa dhati kwa Kristo kwenye misheni Yake; upendo wa dhati unaohitajika kwa wale ambao wamefanya maagano na Mungu.

picha ya mtu akiweka damu ya mwanakondoo kwenye kizingiti cha juu na miimo miwili ya mlango

Damu kwenye Kizingiti na Miimo

Hisopu (mzizi baadaye ulitumika katika utakaso) ilichovywa katika bakuli la damu kutoka kwa mwanakondoo, na kisha damu iliwekwa kwenye kizingiti na miimo ya mlango.

Maana yamkini: Ishara ya kuwatambulisha watu wa Mungu wa agano; utakaso kupitia damu ya Yesu Kristo, ambayo ilimwagwa ili kulipia dhambi zetu.

mkate usiotiwa chachu

Mkate Usiotiwa Chachu

Mkate uliotengenezwa pasipo hamira au chachu nyingine, uwezekano mkubwa ni kutoka kwenye ngano, shayiri, au mtama huko Misri ya kale. Chachu hufanya mkate uwe laini zaidi lakini pia mwepesi zaidi kuoza. Pia, kinyunya kilichotiwa chachu kinahitaji muda kuumuka, hivyo inachukua muda mrefu kutengeneza.

Uliliwa kwa siku saba. Chachu (ambayo ilihusishwa na ufisadi) ilikuwa iondolewe kutoka kila nyumba wakati huu (ona Kutoka 12:19).

Maana yamkini: Usafi; upesi wa kukimbia kutoka utumwani; Kristo kama Mkate wa Uzima (ona 1 Wakorintho 5:7).

bakuli la mizizi

Mizizi michungu

Ilijumuisha saladi, figili, endive, na uwezekano wa mimea mingine yenye ladha chungu.

Ililiwa pamoja na mwanakondoo.

Maana yamkini: Uchungu wa utumwa na kuwa kifungoni huko Misri; uchungu wa utumwa wa kutenda dhambi; uchungu wa kuteseka kwa Kristo kwa ajili ya dhambi zetu.

wanaume wakiwa wamevalia makubadhi pamoja na gongo

Viuno Vimefungwa, Miguuni Wamevaa Viatu , Fimbo Mikononi, Wamesimama Wakati wa Kula

Maana yamkini: Utayari wa kukimbia kutoka utumwani; hamu ya uhuru kutokana na dhambi.

Muhtasari

  1. Ona “Karamu ya Pasaka,” New Era, Apr. 2019, 8–9.

  2. Ona Kutoka 12:22-23; Walawi 14:2-7; Zaburi 51:7.

  3. Ona Kamusi ya Biblia, “Leaven,” Gospel Library.

  4. Ona Kamusi ya Biblia, “Bitter herbs,” Gospel Library.