Liahona
Habari za Shangwe
Machi 2026 Liahona


“Habari za Shangwe,” Liahona, Machi 2026.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Habari za Shangwe

Kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi usio na mwisho, ninajua nitamwona tena rafiki yangu.

Kielelezo cha picha ya wanawake wawili

Kielelezo na Briana Kranz

Kama majirani, Maritza na mimi tulikutana tulipokuwa vijana. Ingawa alikuwa na umri mkubwa zaidi yangu, tulikuja kuwa marafiki wazuri na tulikuwa karibu sana.

Nilipokuwa na miaka 19 na hasa katika uhitaji wa mwelekeo, alinitambulisha kwenye injili ya urejesho ya Yesu Kristo kupitia wamisionari. Tayari nilijua kidogo kuhusu Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kupitia mjomba na bibi yangu. Walikuwa waumini waanzilishi wa Kanisa katika familia yangu.

Maritza alikuwa nami wakati wote wa uongofu wangu, alinisaidia kukuza ushuhuda wangu juu ya Mwokozi na injili Yake, na alinishika kwa mkono kila mara nilipomhitaji.

Nilijifunza kutoka kwake shangwe ya kuishi injili kwa urahisi na kwa kudhamiria. Nilivutiwa na uwezo wake wa kijamii, njia ya kuunganisha familia na marafiki, na uvumilivu katika kufikia malengo ya kimwili na kiroho. Nilijifunza kutoka kwake kwamba tunapokutana na ukweli, lazima tuweke kile tulichojifunza katika matumizi, kushika amri na kutumia mafundisho ya injili katika maisha yetu na familia zetu. Ili kubaki waaminifu, lazima tuwe majasiri katika ushuhuda wetu na kujitahidi kushikilia kwa nguvu imani yetu, licha ya dhiki.

Mwaka 2010, Maritza alifariki katika ajali ya gari. UIlikuwa ni wakati wa kuhuzunisha kwangu, lakini ninajua kwamba kupitia mpango wa wokovu na Upatanisho wa Yesu Kristo, nitamwona tena. Ninajua anaendelea kule alipo sasa kwa mtazamo huo huo wa furaha na msukumo ambao ulimtambulisha yeye hapa duniani.

Ninajua kwamba hii “hali ya kujaribiwa” (Alma 12:24) siyo yote iliyoko. Ninajua tunawaona familia yetu na marafiki tena upande mwingine wa pazia. Tutawaona, tutawasalimu, na kuwa pamoja nao tena. Tutapata uzoefu wa hisia zile zile za upendo tuliokuwa nao kwa kila mmoja duniani (ona Mafundisho na Maagano 130:2). Wanafamilia wangu wapo huko. Ninajua Maritza yupo huko pia.

Maritza kwa furaha alizungumza na kila mtu kuhusu injili hapa duniani. Nina uhakika anafanya vivyo hivyo katika ulimwengu wa roho (ona Mafundisho na Maagano 138:57). Anafundisha kuhusu Upatanisho wa Mwokozi usio na mwisho na habari za shangwe kwamba kwa sababu Yake na kupitia ibada za hekaluni, tunaweza kurudi katika uwepo Wake na uwepo wa Baba ili kuishi kama familia milele.

Muhtasari

  1. Ona Joseph F. Smith, Gospel Doctrine, 5th ed. (1939), 461.