2025
Ushauri Wangu kwa Vijana Wakubwa kuhusu Miadi na Ndoa
Julai 2025


“Ushauri Wangu kwa Vijana Wakubwa kuhusu Miadi na Ndoa,” Liahona, Julai 2025.

Vijana Wakubwa

Ushauri Wangu kwa Vijana Wakubwa kuhusu Miadi na Ndoa

Miadi ni njia mojawapo ya kujua kama mtu fulani ni mtu sahihi kuanza safari ndefu naye.

kielelezo cha mwanaume na mwanamke wakizungumza

Vielelezo na Stephen Neilsen

Ninapenda kufikiria miadi kama chombo.

Vyombo hukusaidia kufikia lengo mahususi. Madhumuni ya kuwa na miadi ni kukuza mahusiano yanayoelekeza kwa ndoa na, kwa nyongeza, kutimiza mpango wa Mungu kwa ajili ya watoto Wake.

Miadi ni njia mojawapo ya kujua kama mtu fulani ni mtu sahihi kuanza safari ndefu naye. Kama Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, alivyofundisha, “Rafiki zangu vijana waseja, tunawashauri mshirikishe uhusiano wenu na watu wa jinsia nyingine katika mipangilio ya miadi ambayo ina uwezekano wa kukomaa na kuwa ndoa.”

Tunapozungumza kuhusu “kwa nini” miadi, tunazungumzia kuhusu kujenga uhusiano wa kudumu pamoja. Tunazungumza kuhusu kujiunganisha sisi wenyewe na kuungana sisi kwa sisi na Mwokozi. Lakini wakati mwingine, kama hatuko makini, tunaweza kuwa tumefokasi sana kwenye kwenda kwenye miadi ili kupata kuwajua watu na kwamba ndoa inakuwa wazo la pili.

Ningependa kuwapa ushauri fulani juu ya jinsi unavyoweza kuboresha uzoefu wako wa miadi. Ushauri wangu mwingi unatokana na uzoefu wangu binafsi, na nina tumaini utakuwa wa msaada kwako.

Fanya Miadi yenye Kusudi

Ikiwa umewahi kuulizwa jinsi unavyofanya miadi , natumaini kwamba “kuwa na kusudi” ni mojawapo ya majibu yako ya kwanza. Acha nijaribu na kuelezea hili kwa mfano.

Zaidi ya nusu muda wa miadi yangu na ya mke wangu ilikuwa ya umbali mrefu. Nilikutana na Catherine tulipokuwa shuleni huko Santiago, Chile. Tulianza kufanya miadi, lakini alihamia nyumbani Antofagasta kabla sijamaliza shahada yangu. Kwa sababu tulitaka uhusiano wetu kukua, mara moja au mara mbili kwa mwezi, nilisafiri kwa basi mwendo wa saa 20 kurudi Antofagasta siku ya Alhamisi mchana, nilitumia mwisho wa wiki na Catherine (ikiwa ni pamoja na ibada za kanisa), na kuchukua basi hilo saa 20 nyingine kurudi Santiago kwa ajili ya darasa langu la 8:00 Jumatatu asubuhi.

Katika siku tusizoweza kuwa pamoja, tuliongea kwenye simu. Kwa kuwa hatukuwa na simu za mkononi wakati huo, nilinunua mpango wa simu ambao uliniruhusu kupiga simu zisizo na kikomo kwenye simu za umma. Nilitumia saa nyingi kwenye kibanda cha simu, na kama mtu mwingine ye yote angehitaji kuitumia, ningelazimika kukata simu na kumwita Catherine punde tu walipomaliza.

Katika uzoefu huu wote, kwa sababu ya vikwazo vingi katika uhusiano wetu, ilibidi nijifunze kuwa na kusudi kuhusu jinsi nilivyowasiliana na Catherine.

Ninawaalika mfanye miadi kwa nia na kwa kukusudia. Rais Russell M. Nelson ametuomba tuwe na makusudi kwa ufuasi wetu. Tunaweza pia kutafuta kuwa wenye kukusudia katika jinsi tunavyofanya miadi.

Tunapaswa kuuliza maswali muhimu:

  • Je, unafikiria nini kuhusu maisha, familia, na muhimu zaidi, Mwokozi?

  • Ninajua ni mambo ya aina gani unayofanya na usiyopenda kufanya, lakini je, unajisikiaje kuhusu injili?

  • Je, ni nini viwango na maadili yako?

Maswali ya kukusudia yanapaswa kuambatana na kufanya shughuli mbalimbali za makusudi. Kuwa na burudani, lakini hakikisha kufanya mambo ya kiroho pamoja pia. Fanya shughuli ambazo zitakusaidia kuelewa na kwa kweli kupata kujuana.

Kielelezo cha pete za harusi

Imani Badala ya Hofu

Baada ya kuwa mmefanya miadi kwa muda, inaweza kuonekana kama uamuzi changamani wa kuchagua kufunga ndoa. Nilikuwa bado na wasiwasi mpaka wakati Catherine na mimi tulipooana!

Kuchagua kufunga ndoa kunaweza kuwa uamuzi mgumu, lakini sio uamuzi unaofanya mara moja tu. Kuchagua kufunga ndoa inamaanisha kuchagua kujiweka upya kwa mwenza wako wa milele katika maisha yako yote na kuimarisha msimamo huo pamoja.

Unapokuwa na maswali kuhusu ndoa au injili, unapaswa “kulichunguza katika akili yako; kisha ni lazima umuulize [Bwana] kama ni sahihi” (Mafundisho na Maagano 9:8) Unapaswa pia kujiuliza mwenyewe, “Je, niko tayari kuchagua kuwa sehemu ya hili kwa maisha yangu yote?”

Nilipofunga ndoa, baadhi ya watu waliniuliza kama nilikuwa na wasiwasi kwamba ningeishia kutalikiana kama wazazi wangu. Jibu langu daima limekuwa hapana. Nilipofunga ndoa, niliamua kwamba ningefanya cho chote kinachohitajika ili kufanya ndoa yangu ifanikiwe. Hiyo ilimaanisha kuchagua kila siku kumfuata Mwokozi na kuwa na ndoa yenye furaha na mke wangu. Nilichagua kutoruhusu hofu ya talaka iniondoe kutoka kwenye uamuzi mzuri na wa haki.

Rais Jeffrey R. Holland, Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, alisema: “Mara baada ya kuwepo na mwangaza halisi, jihadhari na majaribu ya kurudi nyuma kutoka kwenye kitu kizuri. Kama ilikuwa sahihi ulipokuwa ukisali kuhusu hilo na kuamini na kuishi kwa sababu ya hilo, basi ni sahihi hata sasa. Kabiliana na mashaka yako. Shinda hofu yako. “Kwa hivyo usitupe kujiamini kwako.’”

Usisubiri Furaha

Ukweli ni kwamba kuna wengi wenu ambao mna matamanio mazuri na ya dhati ya kumpata mwenza. Unajua hii ni hamu nzuri na ya haki, lakini unapokuwa unahangaika kumpata mtu unayepatana naye, unahisi kukwama katika maendeleo yako kwenye njia ya agano.

Kuhusu hili, Dada Kristen M. Oaks alisema: “Kama utajikuta unatembea papo hapo usubiri matarajio ya ndoa, acha kusubiri na uanze kujiandaa. Jiandae mwenyewe kwa ajili ya maisha—kwa elimu, uzoefu, na mipango. Usisubiri furaha isukumwe kwako. Tafuta fursa za huduma na kujifunza. Na muhimu zaidi, kuamini katika Bwana, ‘kulilingana jina la Bwana kila siku, na kusimama imara katika imani ya yale ambayo yatakuja’ [Mosia 4:11]. Na ninaahidi mnapofanya hivyo, furaha itawajia.

Safari yako kwenye njia ya agano haijakoma kwa sababu bado hujaoa au kuolewa. Bado una muunganiko wako wa kimaagano na Mwokozi. Kama unapambana na kukataliwa, upweke, au hofu, mleteni Yeye katika mapambano yenu. Yeye atakupa msaada. Yeye atakusaidia.

Kwa baadhi, kufanya miadi kwa nia ya kupata mwenza wa milele hakutazaa matunda mara moja. Kwa wengine itafanya hivyo. Bila kujali chochote, ninajua kwamba Mungu atatimiza kila ahadi Yeye aliyoitoa kwetu kama tutakuwa na kusudi na kumtumaini Yeye.

Bila kujali mahali ulipo ulimwenguni au kile kinachotokea au kisichotokea katika maisha yako, kwa sababu ya Yesu Kristo, unaweza kuwa na furaha katika hali zote. Yeye na mafundisho Yake daima ni jibu.

Muhtasari

  1. Dallin H. Oaks, “Choices for Eternity” (worldwide devotional for young adults, Monday, May 21, 2023), Maktaba ya Injili.

  2. “Tunapotafuta kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, juhudi zetu za kumsikiliza Yeye zinahitaji kuwa za dhati zaidi” (Russell M. Nelson, “Msikilize Yeye,” Liahona, Mei 2020, 89).

  3. Jeffrey R. Holland, “Cast Not Away Therefore Your Confidence” (Brigham Young University devotional, Mach. 2, 1999), 4 speeches.byu.edu.

  4. Kristen M. Oaks, “Stand fo Truth,” Maktaba ya Injili.