“Kujibu Swali Kuu: Mwaonaje katika habari ya Kristo?” Liahona, Julai 2025.
Njoo, Unifuate
Kujibu Swali Kuu: Mwaonaje katika habari ya Kristo?
Inaleta tofauti gani katika maisha yajayo jinsi tunavyojibu swali hili?
Kielelezo na David B. Chamberlain
Sehemu ya 76 ya Mafundisho na Maagano inatoa ono linalolenga kwa Kristo, kuwaalika watoto wote wa Mungu kutafakari juu ya swali kubwa, “Mwaonaje katika habari ya Kristo?” (Mathayo 22:42). Mzee Neal A. Maxwell (1926–2004) wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisisitiza umuhimu wa majibu yetu, akisema, “Tunaweza kujibu kwa maisha yetu yote na ndimi zetu, ‘Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai’? (Mathayo 16:16.) Hadi tutakapoweza, cho chote kingine tunachosema na kufanya kitafanya, mwishowe, kuleta tofauti ndogo.”
Wakati wakitafakari maana ya Yohana 5:29, Joseph Smith na Sidney Rigdon walipata ono la mbinguni kuhusu ufufuo wa watoto wa Mungu na falme za utukufu ambazo walipokea kulingana na mwitikio wao kwa Yesu Kristo na injili Yake isiyo na mwisho.
Yesu Kristo ni Nani?
Ono lililoelezwa katika Mafundisho na Maagano 76 linasisitiza kweli muhimu kuhusu Yesu Kristo:
-
“Bwana ni Mungu, na zaidi yake yeye hakuna Mwokozi” (mstari wa 1).
-
Yeye ni “mwenye rehema na neema kwa wale wanaomcha [yeye], na hufurahia kuwaheshimu wale wanao mtumikia [yeye] katika haki” (mstari wa 5).
-
“Alikuja ulimwenguni … kubeba dhambi za ulimwengu, na kuutakasa ulimwengu, na kuusafisha kutokana na udhalimu wote; ili kupitia kwake wote wapate kuokolewa wale ambao Baba aliwaweka katika uwezo wake na kuumbwa naye” (mistari 41–42).
-
Na Yesu Kristo hatimaye “alikamilisha upatanisho huu mkamilifu kwa njia ya umwagaji wa damu yake mwenyewe” (mstari wa 69).
Shahidi Maalumu
Joseph na Sidney kwa ujasiri wanashuhudia ukweli na umuhimu wa Yesu Kristo:
“Yu hai!
“Kwani tulimwona, hata mkono wa kuume wa Mungu; na tukasikia sauti ikitushuhudia kuwa yeye ndiye Mzaliwa Pekee wa Baba—
“Kwamba kwa yeye, na kwa njia yake, na kutoka kwake, dunia zipo na ziliumbwa, na waliomo ni wana na mabinti wa Mungu” (mstari wa 22–24).
Wana wa Upotevu
Yesu Kristo atawaokoa “wote isipokuwa [wana wa upotevu]” (Mafundisho na Maagano 76:44). Wamejibu kikamilifu swali “Mwaonaje katika habari ya Kristo?” kwa kukataa Roho Mtakatifu na kumkana na kumkashifu Yesu Kristo na nguvu Zake baada ya yeye kufunuliwa kwao (ona mstari wa 43). Kwa kufanya hivyo, “wanamsulubisha kwa nafsi zao na kumfedhehesha kwa dhahiri” (mstari wa 35).
Utukufu wa Telestia
Ni kwa jinsi gani wale walio katika ufalme wa telestia hujibu swali “Mwaonaje kwa habari ya Kristo?” Wanachagua kuikataa injili na “ushuhuda wa Yesu” (Mafundisho na Maagano 76:82, 101), na wanakataa amri Zake, wakiwa “waongo, na wachawi, na wazinzi, na makahaba” (mstari wa 103).
Hata hivyo, wanapokea ufufuo na kiwango cha utukufu ambacho “kinapita akili zote” (mstari wa 89). Wanashika angalau sheria moja ya ufalme wa telestia (ona Mafundisho na Maagano 88:36) inayowahitaji wote “kupigia magoti, na kila ulimi utakiri kwake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi milele na milele” (Mafundisho na Maagano 76:110).
Utukufu wa Terestria
Ni kwa jinsi gani wale katika ufalme wa terestria wanajibu swali “Mwaonaje katika habari ya Kristo?” Wakati wanao “ushuhuda wa Yesu,” lakini “hawana ujasiri” ndani yake; “kwa hiyo, hawapati taji juu ya ufalme wa Mungu wetu” (mstari wa 79). Wamebarikiwa kupokea uwepo wa Mwana, lakini siyo utimilifu wa Baba” (mstari wa 77).
Yesu Kristo na injili Yake isiyo na mwisho hutupa changamoto si tu ya kujua bali pia kufanya na kuwa. Ili kupokea utimilifu wa Baba na Mwana, mtu lazima apokee ibada za hekaluni na kuwa mwaminifu kwa maagano hayo. Nabii Joseph Smith anafafanua: “Mtu akipata utimilifu wa ukuhani wa Mungu, ni sharti aupate katika njia ile ile ambayo Yesu Kristo aliipata, na hiyo ilikuwa ni kwa kutii amri zote na kutii ibada zote za nyumba ya Bwana.” Viumbe wa terestria hawako radhi kupokea utimilifu wa Baba.
Utukufu wa Selestia
Wale walio katika ufalme wa selestia wanajibu vipi swali “Mwaonaje katika habari ya Kristo?” Wanapokea “ushuhuda wa Yesu”; wanaamini “katika jina lake;” “wanabatizwa kwa jinsi ya kuzikwa kwake, kwa kuzikwa majini katika jina lake” (mstari wa 51). Wanashika amri [ili] waweze kuoshwa na kusafishwa kutokana na dhambi zao zote, na kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono na yule ambaye ametawazwa na kufungwa kwa uwezo huu” (mstari wa 52). “Wanashinda kwa imani [katika Bwana Yesu Kristo], na kutiwa muhuri na Roho Mtakatifu wa ahadi” (mstari wa 53). “Wanakamilishwa kwa njia ya Yesu aliye mpatanishi wa agano jipya, aliyekamilisha upatanisho huu mkamilifu kwa njia ya umwagikaji wa damu yake yeye mwenyewe.”mstari wa 69
Yesu Kristo anaelewa kazi Yake katika mpango wa Baba wa Mbinguni: “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi” (Yohana 14:6). Hakuna anayepokea utukufu wa selestia au utimilifu wa Baba bila kukubali yote ambayo Mwokozi anatoa kupitia Upatanisho Wake (ona Mafundisho na Maagano 84:37–38): upendo Wake, nguvu, rehema, wema, watumishi, haki, amri, ibada, na maagano.
Rais Russell M. Nelson alisisitiza kazi ya Kanisa la Yesu Kristo katika kuwasaidia watoto wa Mungu kupokea uzima wa milele: “Kusudi la muda mrefu la Kanisa ni kuwasaidia waumini wote kuongeza imani yao katika Bwana wetu Yesu Kristo na Upatanisho Wake, kuwasaidia wao katika kufanya na kushika maagano yao na Mungu, na kuimarisha na kuunganisha familia zao.”
Rais Russell M. Nelson ametuhimiza kufanya ufalme wa selestia kuwa lengo letu la milele, kwa “umakini kufikiria wapi kila moja ya chaguzi [zetu] wakati tukiwa hapa duniani [zitatuweka] katika ulimwengu ujao.” Kwa kujibu mwaliko huu, tutakuwa tayari kujibu swali kuu “Mwaonaje katika habari ya Kristo?”
Ono la viwango vya utukufu linatuhakikishia sio tu kwamba haki ya kujiamulia ipo bali pia kwamba chaguzi ni muhimu. Pia inatukumbusha kwamba, kwa sababu ya Yesu Kristo, sisi “tumekombolewa kutokana na anguko” na “tumekuwa huru milele … kuchagua uhuru na uzima wa milele, kupitia yule Mpatanishi mkuu wa wanadamu wote, au kuchagua utumwa na kifo” (2 Nefi 2:26–27). Tutachagua nini? Kesho yetu katika maisha haya na hatima yetu ya milele ni angavu kama imani yetu katika Yesu Kristo.