“Upendo na Kujali kwa Mwokozi kwa ajili ya yule Mmoja,” Liahona, Julai 2025.
Upendo na Kujali kwa Mwokozi kwa ajili ya yule Mmoja
Tumeombwa kupendana na kutumikiana kama Yesu Kristo anavyofanya—mmoja mmoja.
Kielelezo na Alex Nabaum
Muda mfupi baada ya ubatizo wangu Agosti 1984, nilisikia kuhusu shughuli za burudani pamoja na muziki na nyama choma si mbali na pale nilipoishi Kwekwe, Zimbabwe. Rafiki zangu na mimi tulikuwa na shauku ya kwenda, lakini ilikuwa Jumapili. Marafiki zangu hawakuwa waumini wa Kanisa.
Niliwaambia, “Nitaenda kanisani lakini nitatoroka baada ya mkutano wa sakramenti na kujiunga nanyi.”
Marafiki zangu, ambao walijua udhaifu wangu, walisema, “Kama utafanya hivyo utakosa mambo. Wakati utakapofika, nyama choma itakuwa imeisha!
Nilikuwa na uamuzi wa kufanya. Je, mimi niende kanisani au kwenye nyama choma? Nilichagua nyama choma lakini niligundua Jumapili asubuhi kwamba ilikuwa imefutwa. Wakati huo, nilikuwa nimechelewa sana kwenda kanisani, hivyo nilikaa tu katika chumba changu kidogo cha kupanga.
Mapema mchana huo, nilisikia sauti: “Je, Eddie Dube anaishi hapa?”
Alikuwa rais wangu wa tawi, John Newbold, pamoja na mkewe, Jean. Nilitaka kujificha chini ya kitanda changu! Lakini kabla sijafanya cho chote, walisimama kando ya pazia ambalo lilitenganisha chumba changu kutoka sehemu iliyobakia ya nyumba.
“Ee, Eddie,” walisema, “tulikukosa kanisani leo.”
Tulizungumza kwa muda, na baada ya wao kuondoka, maneno yao ya ukarimu, “Eddie, tulikukosa,” yaliendelea kupita akilini mwangu. Ninawashukuru John na Jean Newbold. Tangu siku hiyo, nimebarikiwa kwa sababu walinisaidia kuona, katika njia binafsi, upendo wa Mwokozi wetu Yesu Kristo na kujali kwa ajili ya yule mmoja.
Mmoja mmoja
Yesu alikuja kama kiumbe aliyefufuka kwa Wanefi baada ya Yeye kuwa na Baba. Yeye alikuja kuwafariji watu. Yeye kwa upendo aliwaalika:
“Inukeni na mje kwangu, ili msukume mikono yenu na muitie kwenye ubavu wangu, na pia kwamba mguse alama za misumari katika mikono yangu na katika miguu yangu, ili mjue mimi ni Mungu wa Israeli, na Mungu wa ulimwengu wote, na nimeuawa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.
“… Na hivi walifanya wakienda mbele mmoja mmoja mpaka walipoenda wote, na waliona na macho yao na kupapasa kwa mikono yao, na walijua ukweli na walishuhudia wenyewe kwamba ni yeye, ambaye manabii waliandika kwamba atakuja” (3 Nefii 11:14–15; msisitizo umeongezwa).
Baadaye, Mwokozi aliwaalika kuwaleta wote waliokuwa wagonjwa, walioumia, au “walioteseka kwa namna yo yote … na akawaponya kila mmoja vile waliletwa kwake” (3 Nefi 17:7, 9; msisitizo umeongezwa). Yeye kisha “aliwachukua [watoto] wadogo, mmoja mmoja, na kuwabariki, na akaomba kwa Baba kwa ajili yao” (3 Nefi 17:21).
Kufikiria kwamba watu 2,500 walikuwa pale hakika inasisimua (ona 3 Nefi 17:25). Nikiwa nimezaliwa na kulelewa katika Afrika, mara nyingi ninaona Mwokozi amesimama katika jua angavu, akisubiri kuponya, kufariji, kuhimiza, na kuonyesha upendo kwa wote walio kuja Kwake. Kama wafuasi Wake, tumeombwa kuwatumikia wale wanao tuzunguka kama Yeye anavyofanya—mmoja mmoja.
Nenda na Imani
Urais wa Muungano wa Usaidizi au akidi ya wazee katika kata au tawi lako, kwa idhini ya askofu au rais wa tawi, umewapangia ninyi watu binafsi na familia za kuwatumikia. Na miongoni mwao unaweza kuwa unawajua kidogo tu. Unaweza kuhisi wasiwasi kuhusu kuwatembelea, kuwapigia simu, au hata kuwatumia ujumbe mfupi. Unaweza kuwa na wasiwasi kwamba hawatakutaka wewe nyumbani kwao. Lakini viongozi wenu kwa maombi wamefikiria kazi hii inaweza kumaanisha nini kwako na baraka zinazoweza kukuletea wewe na familia zako unazo zitumikia. Kwa hiyo, nenda na imani.
Miaka kadhaa iliyopita, nilienda na rais wa kigingi kusini mashariki mwa Marekani kutembelea familia kadhaa kabla ya mkutano wa kigingi. Tulipofika katika nyumba moja, mtu aliyevalia nguo chakavu alitembea hadi kwetu.
“Mnataka nini?” alipiga kelele. “Sitaki watu waje nyumbani kwangu!”
Nilikuwa na wasiwasi wakati mwenendo wa mtu yule ulipoanza kuwa wa kutisha. Nilitaka kumshika rais wa kigingi na kukimbia kurudi kwenye gari! Lakini rais wa kigingi alikuwa mtulivu. “Tunasikitika,” alisema. “Tulidhani askofu wako alikuwa amekuambia kwamba tunakuja.”
Walipokuwa wakizungumza, nilihisi Roho kwa nguvu sana. Nilikusanya ujasiri wangu, nikamkaribia yule mtu, na kusema, “Kaka Mpendwa, Rais Thomas S. Monson [alikuwa nabii wakati ule] amenipa jukumu la kuja hapa. Tuko hapa kukuona wewe. Nimeleta upendo wa nabii kwako.
Nilitazama machoni mwa mtu yule na nikagundua yalikuwa yanatoa machozi. Akaanza kushiriki changamoto zake nasi. Mke wake alimepatwa na msongo wa mawazo. Alikuwa amepoteza kazi yake hivi karibuni. Hakuwa na chakula cha kuwalisha watoto wake. Rais wa kigingi alimhakikishia mtu yule kwamba Kanisa lingemsaidia yeye na familia yake. Tulikuwa na matembezi mazuri.
Wiki kadhaa baadaye, nilimwomba rais wa kigingi kunijulisha hali yake. Aliniambia kwamba askofu wa ndugu huyu na baraza la kata walikuwa wakimsaidia na kwamba yeye na mke wake, ambaye hakuwa muumini wa Kanisa, walianza kukutana na wamisionari.
Utumishi huanza kwa kuwafikia wengine kwa imani na upendo. Tunapokwenda kwa imani, tukimwamini Bwana, tunaweza kutafuta ufunuo kutoka Kwake kuhusu mipango na madhumuni Yake kwa ajili ya uhusiano wetu na kila mmoja wa watoto Wake. Yeye atatusaidia kujua nini cha kusema na kufanya na kutuongoza jinsi ya “kubeba mizigo ya mmoja na ya mwingine, ili iwe miepesi,” “kuomboleza na wale wanao omboleza; … na kuwafariji wale ambao wanahitaji kufarijiwa” (Mosia 18:8–9). Tunapofanya hivyo, tutakuja kujua ni kiasi gani kweli Mwokozi anampenda yule mmoja.
Shangwe Yako Itakuwa Kubwa Jinsi Gani
Hadi siku hii, bado ninawasiliana na John na Jean Newbold. Katika miaka hii yote, ninahisi shangwe kwa sababu ya upendo walionipa. Na wamehisi shangwe kwa kuniona nikiendelea katika injili. Hiki ndicho kinachoweza kutokea tunapotumikia—sisi na wale tunao watumikia tunakuwa karibu na kila mmoja na kuunganika zaidi na Mwokozi.
Mwokozi alifundisha kwamba “thamani ya nafsi ni kubwa machoni mwa Mungu. …
“Na kama itakuwa kwamba utafanya kazi siku zako zote katika kutangaza toba kwa watu hawa, na kuleta, japo iwe nafsi moja kwangu, shangwe yako itakuwa kubwa jinsi gani pamoja naye katika ufalme wa Baba yangu! (Mafundisho na Maagano 18:10, 15; mkazo umeongezwa).
Kama utumishi haukuwa kipaumbele kwako, Rais Russell M. Nelson alifundisha kwamba “sisi sote tunaweza kufanya vizuri zaidi na kuwa bora kuliko hapo awali.” Ninawaalika mbadilike na kugeuza ukurasa mpya. Ninaahidi kwamba unapojihusisha na utumishii, utapata suluhisho la changamoto unazokabiliana nazo kwa sasa.
Ahadi ya Mwokozi ni halisi: “Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza: na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona” (Mathayo 16:25).
Kwa msaada wa Mwokozi, unaweza kuwa aina ya kaka au dada mhudumiaji Yeye anaohitaji uwe kuleta tofauti katika maisha ya watoto wa Baba wa Mbinguni—kila mmoja na kila mmoja mwenye thamani.