Kikao cha Jumapili Mchana
“Tazama Mimi ni Mwangaza Ambao Mtainua Juu”
Dondoo
Mwokozi hajajitoa kutoka katika safari yetu ya duniani. … Mara kwa mara, kwa upendo Wake ulio safi na rehema, Yeye anatusaidia tunapokabiliwa na changamoto za maisha. …
Upendo huo ni dhahiri tunaposaidiana katika kazi Yake.
Tunamkubali nabii wetu aliye hai kwenye mkutano mkuu, na Urais wa Kwanza, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, Viongozi Wakuu wenye Mamlaka na Maafisa wa Kanisa. Kukubali inamaanisha kumwinua mtu mwingine, kumpa usikivu, kuwa waaminifu katika tumaini lao, kuyafanyia kazi maneno yao. Wananena kwa mwongozo wa Bwana, wanaelewa mambo yalivyo sasa, kushuka kwa maadili ya jamii, na jitihada za adui zinazoongezeka za kuzuia mpango wa Baba. Katika kuinua juu mikono yetu, tunaahidi kumuunga mkono, si tu kwa wakati ule bali katika maisha yetu ya kila siku. …
… Sisi tunainua juu nuru ya Bwana wakati tunaposhikilia kwa nguvu maagano yetu na tunapomuunga mkono nabii wetu aliye hai wakati anaponena maneno ya Mungu. …
Kumwinua nabii ni kazi takatifu. Hatukai tu kimya bali kwa kujishughulisha tunamtetea, kufuata ushauri wake, kufundisha maneno yake na kumwombea. …
Akina kaka na akina dada, tunahitaji kuinua zaidi na kunung’unika kidogo, kuinua zaidi neno la Bwana, njia Zake, na nabii Wake. …
… Tunapomkubali nabii wetu, tunashuhudia yeye ameitwa na Mwokozi wetu, ambaye ni “nuru … ya ulimwengu.”