Kikao cha Jumamosi Jioni
Shangwe ya Ukombozi Wetu
Dondoo
Kutubu kunaturuhusu kuhisi upendo wa Mungu na kumjua na kumpenda Yeye katika njia ambazo kamwe hatungeweza kuzijua. …
Ninajua kwamba Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, ni mwenye nguvu ya kuokoa. …
Unaweza kuhisi wakati mwingine kwamba haiwezekani kukombolewa, kwamba pengine wewe umetengwa na upendo wa Mungu na nguvu ya upatanisho ya Mwokozi kwa sababu ya kile unachopambana nacho au kwa sababu ya kile ulichokifanya. Lakini ninashuhudia kwamba hauko chini ya ufiko wa Bwana. …
Tunapoishi maagano yetu, Bwana anaweza kutupatia msaada na nguvu tunazohitaji ili kutambua na kushinda udhaifu wetu, ikijumuisha vimelea vya kiroho vya kiburi. …
… Hitaji letu la uponyaji na msaada si mzigo Kwake, bali ndiyo sababu hasa ya Yeye kuja. …
Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wanakuona. Wanaujua moyo wako. Wanajali kuhusu kile unachokijali, ikijumuisha wale unaowapenda. …
Ikiwa unapambana na hali unayodhani ulipaswa kuwa umeishinda kwa sasa, usikate tamaa. Kuwa mvumilivu kwako mwenyewe, shika maagano yako, tubu mara kwa mara, tafuta usaidizi wa viongozi wako kama itahitajika na nenda kwenye nyumba ya Bwana mara kwa mara kadiri uwezavyo. Sikiliza na utii ushawishi anaokutumia. Yeye hataacha uhusiano Wake wa agano na wewe. …
Kila siku ni siku mpya iliyojawa na tumaini na uwezekano kwa sababu ya Yesu Kristo.