Kikao cha Jumapili Mchana
Lisha Mizizi, na Matawi Yatakua
Dondoo
Mojawapo ya mambo muhimu tunayoweza kujifunza katika maisha haya ni tofauti kati ya kile ambacho ni cha milele na ambacho si cha milele. …
… Baadhi ya kweli ni za msingi, za muhimu, katika mizizi ya imani yetu. Zingine ni viambatisho au matawi—yenye thamani, lakini pale tu yanapounganishwa kwenye misingi. …
Kwa maneno mengine, Yesu Kristo na dhabihu Yake ya upatanisho ni mizizi ya ushuhuda wetu. Vitu vingine vyote ni matawi. …
Linapokuja suala la kulisha shuhuda zetu juu ya Yesu Kristo, ninajiuliza kama wakati mwingine tunachanganya matawi kuwa mizizi. …
Lazima tujiulize: Je, ushuhuda wangu unategemea kile ninachotumaini kitokee katika maisha yangu? Je, unategemea matendo au mitazamo ya wengine? Au je, umejengwa imara juu ya Yesu Kristo, “umekita mizizi na kujengwa ndani yake” [Wakolosai 2:7], bila kujali hali za maisha zinazobadilika? …
Hatupaswi kutarajia kuelewa kila kitu kabla ya kutenda. Hiyo si imani. … Tukisubiri mpaka maswali yetu yote yajibiwe ndiyo tutende, tunazuia vikali mema tunayoweza kutimiza, na tunazuia nguvu ya imani yetu. …
Imani huvumilia majaribu na mashaka ya maisha kwa sababu imekita mizizi katika Kristo na mafundisho Yake. Yesu Kristo na Baba yetu wa Mbinguni Aliyemtuma, kwa pamoja wanajumuisha lengo moja lililonyooka, la kuaminika la tumaini letu. …
Ni sala yangu ya dhati na baraka zangu kwamba daima tutarutubisha mizizi ya imani yetu katika Mwokozi, katika mafundisho Yake na katika Kanisa Lake.