2024
Kuzika Silaha Zetu za Uasi
Novemba 2024


Kikao cha Jumamosi Mchana

Kuzika Silaha Zetu za Uasi

Dondoo

bango

Pakua PDF

Uasi unaweza kuwa wa wazi au kimyakimya. …

Pengine aina ya uasi wa kuchukiza zaidi dhidi ya Mungu, hata hivyo, ni ule wa kimyakimya—kupuuza mapenzi Yake katika maisha yetu. Wengi ambao kamwe hawangeweza kuonyesha uasi wa wazi bado wanaweza kupinga mapenzi na neno la Mungu kwa kufuata njia yao wenyewe bila kujali maelekezo ya kiungu. …

Panga na silaha zingine ambazo Walamani waongofu walizizika zilikuwa silaha za uasi kwa sababu ya jinsi walivyozitumia. Aina hizo hizo za silaha mikononi mwa watoto wao, zikitumika katika ulinzi wa familia na uhuru, hazikuwa silaha za uasi dhidi ya Mungu hata kidogo. …

Kwa njia sawa na hiyo, kuna mambo katika maisha yetu ambayo yanaweza kuwa vuguvugu au hata mazuri lakini ambayo yakitumiwa kwa njia isiyo sahihi huwa “silaha za uasi.”

… Ikiwa upendo wetu kwa Mungu na msimamo wetu wa kumtumikia kwa uwezo wetu wote, akili na nguvu zetu zote vitakuwa kigezo ambacho kwacho tunapima vitu vyote na kufanya maamuzi yetu yote, tutakuwa tumezika silaha zetu za uasi. Kwa neema ya Kristo, Mungu atasamehe dhambi zetu na uasi wa zamani na ataondoa doa la dhambi hizo na uasi huo kutoka kwenye mioyo yetu.

Kuzika silaha zetu za uasi kunaleta shangwe ya kipekee. … Na tuzike—chini, chini kabisa—dalili yoyote ya uasi dhidi ya Mungu katika maisha yetu na tuibadilishe kwa moyo wa hiari na akili iliyo tayari.