2024
Bwana Yesu Kristo Atakuja Tena
Novemba 2024


Kikao cha Jumapili Mchana

Bwana Yesu Kristo Atakuja Tena

Dondoo

bango

Pakua PDF

Bwana hakika anaharakisha kazi Yake.

Kwa nini tunajenga mahekalu kwa kasi kama hiyo? Kwa nini? Kwa sababu Bwana ametuagiza kufanya hivyo. Baraka za hekalu husaidia kukusanya Israeli pande zote mbili za pazia. Baraka hizi pia zinasaidia kuwaandaa watu ambao watasaidia kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Bwana! …

Hapa ni ahadi yangu kwenu: Kila mtafutaji wa dhati wa Yesu Kristo atampata hekaluni. …

Nimejifunza kwamba swali muhimu zaidi ambalo kila mmoja wetu lazima alijibu ni hili: Kwa nani au kwenye nini nitayatoa maisha yangu?

Uamuzi wangu wa kumfuata Yesu Kristo ni uamuzi muhimu zaidi ambao nimewahi kuufanya. … Umenisaidia pia kushinda dhoruba za maisha. …

Ninawasihi mtenge muda kila wiki—kwa maisha yenu yote yaliyosalia—kuongeza uelewa wenu wa Upatanisho wa Yesu Kristo. …

Yesu Kristo alijichukulia juu Yake dhambi zako, maumivu yako, kuvunjika moyo kwako na madhaifu yako. Huna Haja ya kuyabeba peke yako!

Si mapema sana wala hujachelewa sana kwa wewe kuwa mfuasi mcha Mungu wa Yesu Kristo. …

Mazuri zaidi bado yako mbeleni, wapendwa kaka zangu na dada zangu, kwa sababu Mwokozi anakuja tena! Mazuri zaidi bado yako mbeleni kwa sababu Bwana anaharakisha kazi Yake. Mazuri zaidi bado yako mbeleni kadiri tunavyoigeuza mioyo yetu na maisha yetu kwa Yesu Kristo.